HALMSHAURI Halmashauri ya Chalinze yapata vifaa vya kisasa vya kupima Ardhi, Sasa kupima viwanja 1000 kwa wiki

 


NA ANDREW CHALE, CHALINZE.

HALMASHAURI ya Chalinze, imepokea Vifaa  vipya na vya kisasa vya kupimia Ardhi ili kuwezesha upimaji wa Viwanja na kupanga miji ya Halmashauri hiyo kuwa ya kisasa.


Tukio hilo limeshuhudiwa na viongozi mbalimbali likiongozwa na  Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ramadhani Possi, Mwenyekiti wa Halmashauri Geoffrey Kamugisha, Mbunge wa jimbo hilo, Ridhiwani Kikwete pamoja na baadhi ya Madiwani waliweza kuonesha furaha yao katika kuona Ardhi inakwenda kupimwa hali itakayoongeza thamani ya Ardhi.


Awali akizungumza wakati wa kuvipokea vifaa hivyo, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ramadhani Possi alisema zitawasadia kwendana na kasi la upimaji wa Ardhi ambayo inaenda kupimwa yote ilikuendelea kuvutia Waekezaji.


"Lengo kuendelea kuvutia uwekezaji na moja wapo ni kuwa na ardhi iliyopimwa. Wawekezji watakaokuja kwenye Halmashauri yetu lazima tuwe na ardhi iliyopimwa.  


Kupitia vifaa hivi tutaendelea kupima viwanja vya makazi, viwanja vya biashara, pamoja na vya viwanda." Alisema Mkurugenzi Ramdhani Possi.


Aidha, aliongeza kuwa, wamejipanga kwenda kupima viwanja hivyo wakaamua kununua kifaa hicho cha kisasa kitakachosaidia Halmashauri.


"Tumesema ili twende na  kasi ya upimaji kwa haraka, Kama Halmashauri tumenunua hiki kifaa kwa Tshs. Milioni 38 kwa sasa naona tunaenda kuona mwanga mzuri, Maana huwezi kupima viwanja bila kuwa na hiki kifaa." Alisema Mkurugenzi huyo, Ramadhani Possi.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Geofrey Kamugisha alishukuru ununuzi wa Vifaa na kwamba unaleta ukombozi mpya kwa Chalinze.


Nae Mbunge wa Jimbo hilo, Ridhiwani Kikwete  alishukuru Ofisi ya Mkurugenzi kwa kutekeleza maagizo ya Baraza la Madiwani na maagizo ya Viongozi. 


"Mashine hii  ya kupima na kupanga ardhi imekuja wakati muafaka. Zamani Wapima wetu waliweza kupima na kuchora viwanja Vitano (5) hadi Kumi (10) kwa Siku. 


Ujio wake itawezesha Halmashauri kupima viwanja 150 hadi 200 kwa Siku sawa na viwanja 1000 kwa Wiki." Alisema Ridhiwani Kikwete.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala na fedha wa kampuni ya Global Survey, Abdul Mlanzi  alibainisha kuwa, kifaa hiko kinachofahamika kama Real Time Kainematik (RTK) ni cha kisasa ambapo kina  uwezo wa kupima viwanja kuanzia hadi 100 hadi 200 kwa siku.


"Kampuni yetu pia itaendesha mafunzo maalum ya junsi ya kuvitumia na kuviendesha kwa watumishi idara ya ardhi wa Halmshauri.


Vifaa hivi vipo katika mfumo wa kisasa ambapo duniani kote wanatumia hususani nchi zilizoendelea" alisema Abdul Mlanzi.


Kwa upande wao baadhi ya Madiwani walioshuhudia tukio hilo walibainisha kuwa, Chalinze inaenda kumaliza tatizo la migogoro ya ardhi huku wakitarajia  kupanmda thamani viwanja vinapoenda kupimwa.







Post a Comment

0 Comments