Apr 17, 2021

Rais Samia awatunuku kamisheni maafisa JWTZ

  Muungwana Blog       Apr 17, 2021

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewatunuku Kamisheni Maafisa wanafunzi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ).


Hafla hiyo imefanyika katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma, ambapo maafisa mbalimbali wa JWTZ wametunukiwa kamisheni baada ya kukamilisha mafunzo yako katika nchi mbalimbali.


Kozi hiyo imehusisha jumla ya maafisa wa Sayansi ya Kijeshi 386 ambapo kati yao wanawake ni 51 na wanaume ni 335. Maafisa wahitimu 143 ni kutoka kundi la kwanza kwa mwaka 2017 na kundi la mwaka 2020 limehusisha maafisa wahitimu 226 pamoja na maafisa 7 wahitimu kutoka nchi rafiki.

logoblog

Thanks for reading Rais Samia awatunuku kamisheni maafisa JWTZ

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment