Apr 17, 2021

Ufugaji bora wa bata mzinga

  Muungwana Blog       Apr 17, 2021

 

Bata mzinga wanahitaji matunzo ya hali ya juu. Kwa kawaida bata mzinga hula chakula kingi kuliko kuku. Bei yake ni ghali zaidi. Kabla ya kuanza ufugaji wa bata mzinga ni lazima kuhakikisha una chakula cha kutosha kwa sababu ulishaji wa ndege hawa kadri wanavyokua huwa na gharama kubwa zaidi.

Ni muhimu pia kujifunza kwa undani na kufahamu namna ya kutunza vifaranga wa bata mzinga kwa kuwa hufa kwa urahisi sana. Pia, unapaswa kujikita kutafuta soko kwa sababu wanapokuwa ni vigumu kuwatunza kwa muda mrefu kutokana na ukubwa wa gharama ya chakula.

Wafugaji wachache kati ya wengi waliojaribu kuwafuga ndege hawa na kufanikiwa hata kufikia malengo yao ni kutokana na kuzingatia lishe kamili. Pamoja na hayo, wapo wafugaji ambao walishindwa kutokana na magonjwa pamoja na gharama ya utunzaji.

Banda 
Ni vyema banda liwe limesakafiwa au banda la asili la udongo usiotuhamisha maji. Pia, unaweza kutumia banda lenye mbao au mabanzi kwa chini. Unaweza pia kutandaza maranda kwenye mabanda. Hakikisha kuta za banda zimefunikwa vizuri ili kuwakinga dhidi ya baridi.

Chakula.
Chakula cha bata mzinga hakina tofauti na cha kuku. Vifaranga wanahitaji kupata lishe kamili yenye protini kwa wingi ili waweze kukua vizuri. Vifaranga kwa siku za awali wanahitaji kiasi cha asilimia 27 ya protini mpaka wanapofikia umri wa wiki sita.

Baada ya hapo mfugaji anaweza kupunguza hadi kufikia asilimia 18, na kuendelea hivyo hadi wanapokomaa.  Kutokana na gharama ya kununua chakula kuwa kubwa, unaweza kutumia reseheni ifuatayo kwa ajili ya kutengeneza chakula cha bata mzinga wewe mwenyewe.

Mahitaji.
Mahindi 5kg (yasiyokuwa na dawa), Karanga 5kg, Dagaa 5kg, Mashudu 10kg, Chokaa 5kg (chokaa inayotumika kwa lishe ya mifugo) . Namna ya kutengeneza chakula Twanga au saga pamoja kiasi kisha walishe vifaranga. Mchanganyiko huu hutegemeana na wingi wa bata mzinga unaowafuga. Hakikisha kila bata anapata chakula cha kutosha na chenye uwiano ulioelekezwa.

Pia waangalie mara kwa mara kuhakikisha wana chakula cha kutosha.
Uhifadhi: Hifadhi chakula cha ziada kwenye mifuko au debe kisha weka sehemu isiyo na unyevu.

Kutaga
Bata mzinga huanza kutaga anapofikisha umri wa mwaka mmoja. Ndege hawa wana uwezo wa kutaga kati ya mayai 15 hadi 20 kwa mara ya kwanza na kisha kuhatamia. Anapoendelea kukua huweza kutaga hadi mayai 30. Hii ni kulingana na lishe nzuri atakayopatiwa.

Kuhatamia.
Bata mzinga anaweza kuhatamia mayai 17 hadi 20. Mayai hayo huhatamiwa kwa siku 28 na huanza kuanguliwa vifaranga kwa muda wa siku 3, kuanzia siku ya 28 hadi 31. Baada ya hapo mayai yaliyosalia bila kuanguliwa hutakiwa kutupwa kwa kuwa hayatoanguliwa tena na hayafai kwa matumizi mengine.

Jinsi ya kulea vifaranga vya bata mzinga.
Vifaranga Wa bata mzinga ni tofauti na wa kuku, wakuku hutotolewa tayari wanajua kujifunza kula na kunywa Maji wakati Wa bata mzinga huzubaa kwa siku kama 4 ndipo wajue kula vizuri hivya wana hitaji uangalizi Wa hali ya juu sana. Hukaa kwenye brooder kwa muda Wa wiki 4 ambapo watahitaji joto la kutosha muda wote ambapo wiki ya kwanza watahitaji nyuzi joto 38 na na wiki ya pili utapunguza nyuzi joto 5 kila wiki utapunguza nyuzi joto 5. wanakuwa kwa haraka hivyo wanahitaji sehemu Kubwa ya kuwalea sentimita 20×20 kwa kila kifaranga kwenye wiki ya pili hadi ya Tatu.

Wanahitaji Chakula chenye protini nyingi 28% katika Chakula chao kwa wiki 8 za mwanzoni hivyo ni bora kuwapa broiler starter kwa muda Wa miezi miwili. Maharisho ya sehemu ya kuwale (brooder) yanatakiwa yazingatie mambo yafuatayo: Kuwe kuna matandiko chini ya kutosha kiasi cha kina cha inch 3 ili kuweka hali ya joto. Matandiko yaweza kuwa maranda nyasi pumba za mpunga. Weka vyombo vya kulia Chakula na kunywea Maji kabla hujawaingiza Vifaranga hao.

Weka vitu vya kung’aa katika Chakula na Maji ili kuwa vutia kujifunza kula.Vitu vya kung’aa yaweza kuwa gololi zile za kuchezea watoto unatumbukiza kwenye Maji hivyo zile Rangi zitawavutia kusogea pale na kudonoa donoa au weka Maji ya Mchele kama Maji yao ya kunywa ile Rangi nyeupe itawavutia kusogelea Maji hii ni namna ya kuwafunza kula au wachanganye na Vifaranga Wa kuku watajifunza kula kupitia Vifaranga Wa kuku.

Wape Chakula muda wate na wape Majani wiki ya pili maana 50% ya Chakula chao ni Majani Mboga Mboga mbichi. Wape joto kwa vyanzo vya joto ulivyo navyo kama taa za umeme 100w au 200w jiko la Mkaa taa ya chemli au kandiri au tumia Njia za asili. Kama ilivyo kwa kuku bata mzinga wanahitaji Dawa na chajo.

Wiki ya kwanza wape Newcastle vaccine wiki ya 4 wape fowl pox vaccine (ndui) wiki ya 6 wape Newcastle vaccine Utarudia baada ya miezi mitatu mitatu chanjo hii ya Newcastle.Wape vitamini na madini katika Chakula chao.

Ikifika wiki ya 8 unaweza kuanza kuwatoa nje wajifunze mazingira ya nje na kujitafutia maana bata mzinga ni watafutiaji Chakula wazuri kama kuku Wa kienyeji japo hupenda sana Majani. Ni vizuri kuwapa lusina mbichi hufanya vizuri katika bata mzinga. Wiki ya 24 hadi 28 wanakuwa tayari wana kilo 8 hadi 12 hivyo wanaanza kutaga wachanganye na maduma katika ratio ya 1:5 yani dume 1 majike 5 hii ni kama bado hawajawa wazito sana kama wameshakuwa wazito au kuanze kuwa wavivu kuzeeka wawekee ratio ya 1:3 yani dume 1 majike 3.Bata mzinga hutaga kwa msimu kama walivyo kanga na hulalia siku 28 kama kanga na wanauwezo wakulalia Mayai yao 10 hadi 15 lakini hutaga mengi zaidi hivyo nivizuri ukatumia Mashine ya kutotolesha au kama una kuku Wa kienyeji anapo lalia unamuwekea ya bata mzinga Mayai 6.

Hivyo wakati huo bata anaendelea kutaga huku kuku wanalalia Mayai yao.Hivyo ni Njia nzuri maana bata mzinga wanatabia ya kususa Mayai yao km MTU ukiyashika na marashi au yakipata harufu ambayo sio yake.

Maji
Kama ilivyo ndege wengine, bata mzinga pia wanahitaji kupatiwa maji masafi na ya kutosha wakati wote. Wawekee maji katika chombo ambacho hawatamwaga na wanakifikia vizuri. Hakikisha maji hayamwagiki bandani kwani kwa kufanya hivyo banda litachafuka na kukaribisha magonjwa kwa urahisi. Ni vizuri kuwalisha bata mzinga vyakula vingine kama majani. Majani husaidia kuwapatia protini: mfano; kunde, fiwi na aina nyingine za majani jamii ya mikunde huhitajika zaidi kwa kiasi cha 25% hadi 30%.

Magonjwa
Bata mzinga hushambuliwa na magonjwa kama taifodi, mafua na kuharisha damu. Wanapougua ni rahisi kuambukiza kuku, bata na ndege wengine wanaofugwa kwa haraka sana. Pia, ndege hawa husumbuliwa na viroboto wanaosababishwa na uchafu wa banda hasa linapokuwa na vumbi.

Chanjo.
Bata mzinga wanatakiwa kupatiwa chanjo ya ndui (mara moja kila mwaka), kideri (kila baada ya miezi mitatu), gumboro (kwa muda wa wiki tano – ukiwapa jumatatu, basi unawapatia kila jumatatu ya wiki), na vitamini A mara baada ya kuanguliwa.
logoblog

Thanks for reading Ufugaji bora wa bata mzinga

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment