Afrika Kusini yabaini kesi za kwanza za kirusi kipya cha India

 


Wizara ya afya ya Afrika Kusini imeripoti visa vinne vya kwanza vya aina mpya ya kirusi cha corona kilichogunduliwa nchini India. 

Kwenye taarifa yake wizara ya afya pia imebaini visa 11 vya kirusi kilichobainika mara ya kwanza Uingereza. Maambukizi ya kirusi kipya cha India yamepatikana katika majimbo ya Gauteng na Kwazulu Natal na watu hao walikuwa wamesafiri kutoka India. 

India jana imeorodhesha kiwango cha juu cha vifo 4,187 vya Covid-19 ikiwa ni rekodi ya juu ndani ya siku moja. 

Afrika Kusini ndio nchi iliyoathirika zaidi na janga la corona barani Afrika kulikochangiwa na wimbi la pili la aina mpya ya kirusi kilichokuwa kikienea kwa kasi. 

Hadi kufikia sasa Afrika Kusini imeagiza mamilioni ya dozi za chanjo ya Johnson & Johnson na Pfizer ili kuongeza kasi ya kampeni yake ya utoaji chanjo. 

Kati ya wakaazi wake milioni 60, ni wahudumu wa afya wapatao laki 3 pekee waliopatiwa chanjo.


Post a Comment

0 Comments