May 8, 2021

Breaking News: Mchezo wa Simba na Yanga kutochezwa

  Muungwana Blog 3       May 8, 2021


 BAADA ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga kupelekwa mbele kikosi cha Yanga kimewasili uwanjani kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku.

Muda wa awali ulipangwa saa 11:00 ila taarifa ambayo imetolewa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imepeleka mbele muda mpaka saa 1:00 usiku.

Wachezaji wa Yanga wameanza mazoezi na wameweka wazi kuwa ikifika dakika 15 watawasubiri wapinzani wao ili kuona kama Simba watafika au la.

Baada ya kumaliza kufanya mazoezi mepesi, kikosi cha Yanga kimerejea ndani huku kikosi cha Simba kikiwasili uwanjani wakati huu.

Pia baadhi ya mashabiki wameanza kutoka uwanjani kwa maelezo kuwa wameshindwa kwenda na wakati.

logoblog

Thanks for reading Breaking News: Mchezo wa Simba na Yanga kutochezwa

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment