May 4, 2021

Bunge la Uganda lapitisha sheria kuhusu uhalifu wa kijinsia


Bunge la Uganda limepitisha sheria ya kina kuhusu uhalifu wa kijinsia, ikifuta baadhi ya vifungu katika sheria ya jinai ya miongo kadhaa.

Hatua hiyo mpya inatoa nafasi ya kubuniwa kwa sajili ya kitaifa ya wahalifu wa kingono.

Mtu yeyote atakayefungwa kwa kuwa mhalifu wa kingono jina lake litaorodheshwa katika sajili hiyo ndani ya siku kumi ya mahakama kutoa hukumu yake.

Watalazimika kutoa maelezo kuhusu historia yao wakati wa kuomba nafasi ya kazi, au nafasi yoyote ambayo inawaweka hatarini watoto wanaowatunza.

Na kwa mara ya kwanza, sheria juu ya unyanyasaji mitaani, unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya umma na vile vile unyanyasaji katika mazingira ya kitaalam imeanzishwa.

Sheria hiyo pia inatoa adhabu yaya kifungo cha miaka saba gerezani kwa mtu yeyeote atakayesambaza video zilizo na maudhui ya kiutuuzima katika mitandao ya kijamii.

Wanaharakati wanasema sheria hiyo itasaidia kukabiliana na visa vya watu kuvujisha video za ngono kama hatua y akumhujumu muathiriwa, katika baadhi ya visa video kama hizo zinasambazwa kutoka kwa akaunti ya muathirika.

sheria hiyo mpya pia inaharamisha utalii wa kingono unaohusisha watoto.

KWA HABARI ZAIDI <DOWNLOAD HAPA>
Share:
Loading...

Popular Posts

Copyright © MUUNGWANA BLOG | Powered by Blogger