China imesema sehemu kubwa ya mabaki ya roketi yake yameungua ilipoingia

 


Mamlaka ya anga ya China imesema sehemu muhimu ya roketi yake kubwa aina ya Long March 5B iliwasili katika uso wa dunia katika eneo la Maldives usawa wa Bahari ya Hindi na kwamba kwa kiasi kikubwa imeungua.

Mtaalamu wa masuala ya anga wa Havard, Jonathan McDowell, aliekuwa akifuatilia kuanguka kwa sehemu ya roketi hiyo, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba kwa kawaida kuingia katika eneo la dunia kwa roketi hiyo kuna mahesabu yake. 

Lakini kilichotokea ni uzembe.Nae Mratibu wa kituo cha safari za anga za juu cha Marekani-NASA Bill Nelson alitoa taarifa inayosema: "Ni wazi kwamba China inashindwa kufikia viwango vya uwajibikaji kuhusu mabaki katika eneo lao anga.


Post a Comment

0 Comments