Rais wa shirikisho la soka Ujerumani Keller ahimizwa kujiuzulu

 


Rais wa shirikisho la kandanda Ujerumani - DFB Fritz Keller anakabiliwa na wito wa kumtaka ajiuzulu baada ya kumlinganisha mmoja wa mamakamu wake na jaji aliyekuwa na sifa mbaya wa enzi ya Manazi Roland Freisler. 

DFB imesema jana kuwa marais wa vyama vyake vya majimbo na mikoa walipiga kura ya kutokuwa na imani na Keller mwenye umri w amiaka 64 na kumtaka ajiuzulu ili kuepusha uharibifu zaidi kwa shirikisho hilo. 

Katika mkutano usio wa kawaida ulioandaliwa mwishoni mwa wiki mjini Potsdam, vyama hivyo pia viliondoa imani yao kwa katibu mkuu Friedrich Curtius, ambaye amekuwa katika mgogoro wa muda mrefu wa madaraka na Keller. 

Taarifa ya DFB imesema vyama vya kandanda Ujerumani vinalaani kauli aliyotoa Keller mnamo Aprili 23 kwa kumlinganisha makamu wa rais Rainer Koch na jaji wa manazi Freisler.


Post a Comment

0 Comments