May 9, 2021

Tetesi za soka Ulaya leo

  Muungwana Blog 2       May 9, 2021

Ajax inajiandaa kupambana na Manchester United kumpata winga wa Ghana, Kamaldeen Sulemana, ambaye sasa anaichezea FC Nordsjaelland ya Denmark. (Mail on Sunday)


Manchester United itampa mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani nyongeza ya mshahara wa pauni milioni 2.5 ili kumbakiza mchezaji huyo wa miaka 34 klabuni hapo kwa mwaka mwingine.(Sun on Sunday)


Declan Rice wa West Ham amedokeza kwamba anaweza kuondoka klabuni hapo kutafuta nafasi Manchester United na Chelsea waliokuwa wakimfuatilia kwa muda mrefu kiungo huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 22. (Sunday Mirror)


Mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane ndiye anayewindwa sana na Chelsea, ambao "wako tayari kupanga zabuni kubwa" kwa mchezaji huyo wa miaka 27 ikiwa kuna dokezo mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza anaweza kupatikana. (Football Insider)

Nahodha wa England Kane yuko tayari kumwomba mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy kuzingatia ofa zake kwa msimu huu wa joto. (Sun on Sunday)


Manchester United wanapenda kumsajili kiungo wa England Jude Bellingham, 17, kutoka Borussia Dortmund msimu huu wa joto badala ya mwenzake Jadon Sancho, 21.(Bild, via Manchester Evening News)

Bellingham, hata hivyo, anafurahia huko Dortmund, ambaye "hakika hawatamuuza" kijana huyo. (Sport 1 journalist Patrick Berger on Twitter)


Borussia Dortmund pia hawataki kumuuza mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 20, na watazingatia tu ofa za euro 180m kwa kijana huyo wa miaka 20. (Marca)


Washika bunduki wanapenda kumnasa winga wa Kiingereza mwenye umri wa miaka 18 Kido Taylor-Hart kwa makubaliano mapya mwezi ujao. (Sun on Sunday)


Newcastle United imeongeza kandarasi ya beki wa Uswisi Fabian Schar, na mchezaji huyo wa miaka 29 kutokana na mkataba wake kumalizika mwaka 2022. (Blick via Chronicle Live)


Everton inaweza kumsajili mlinda mlango wa zamani wa Poland na Arsenal Wojciech Szczesny kutoka Juventus msimu huu wa joto lakini Paris St-Germain pia inavutiwa na mchezaji huyo wa miaka 31. (Calciomercato - in Italian)


Kiungo wa kati wa Sheffield United, 23, Sander Berge, ambaye amekuwa akihusishwa na Arsenal, Aston Villa na Everton, anaweza kuondoka Bramall Lane kwa pauni milioni 35 kwa sababu ya kifungu cha kushuka daraja katika mkataba wake. (Yorkshire Live)


West Ham wanatafuta kumsajili tena mshambuliaji Marko Arnautovic kutoka klabu ya China ya Shanghai SIPG, wakati Crystal Palace, Everton, Inter Milan na AC Milan pia wamehusishwa na mchezaji huyo wa Austria mwenye umri wa miaka 32. (Il Resto del Carlino, via Sunday Mail)


Chelsea inataka kumsajili mshambuliaji wa miaka 19, Armando Broja kwa mkataba wa muda mrefu huko Stamford Bridge baada ya kuvutiwa na mchezaji huyo wa Albania anayecheza kwa mkopo Vitesse Arnhem. (Sun on Sunday)


Kocha mpya wa Roma Jose Mourinho anaweza kuangalia uwezekano wa kumleta mshambuliaji wa Italia Andrea Belotti mwenye umri wa miaka 27 kutoka Torino, na mshambuliaji wa Paris St-Germain wa Argentina Mauro Icardi pia ni shabaha yake. Roma pia inaweza bado kubaki na mshambuliaji wa Bosnia mwenye umri wa miaka 35 Edin Dzeko, ambaye hapo awali alitarajiwa kuondoka klabuni hapo majira ya joto. (Corriere dello Sport - in Italian)


Barcelona bado wanavutiwa na Ryan Gravenberch wa Ajax, 18, baada ya kujaribu kwanza kusaini kiungo huyo wa Uholanzi akiwa na umri wa miaka 15. Barca, hata hivyo, inakabiliwa na ushindani kwa Gravenberch, ambaye amekuwa akihusishwa na vilabu kadhaa zikiwemo Manchester United na Juventus. (Mundo Deportivo - in Spanish)


Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amemhakikishia kiungo wa kimataifa wa Japan Takumi Minamino, 26, ambaye amekuwa kwa mkopo huko Southampton, kwamba bado atasalia Anfield. (Goal)

 

logoblog

Thanks for reading Tetesi za soka Ulaya leo

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment