https://monetag.com/?ref_id=TTIb “Tunaandaa sheria ya faragha kulinda taarifa za mtumiaji” Ndugulile | Muungwana BLOG

“Tunaandaa sheria ya faragha kulinda taarifa za mtumiaji” Ndugulile


Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Faustine Ndugulile amesema katika kutengeneza mazingira rafiki na wezeshi ya sekta ya Teknolojiaya Habari na Mawasiliano TEHAMA, anakusudia kutunga sheria ya faragha.

Pia ametoa wito kwa wadau kupeleka mawazo, maoni au ushauri na namna ya kuboresha sekta hiyo nchini.

Ndugulile ametoa kauli hiyo katika mdahalo wa wadau wasekta ya TEHAMA ambao pamoja na mambo mengine ulilenga kujadili changamoto na suluhisho kuhusu sekta ya Mawasiliano na Tekbnolojia nchini.

Akizungumza katika mdahalo huo uliokuwa na mada kuu kuhusu mapinduzi ya nne ya viwanda kwa uchumi wa dijitali wa ushindani, Dk. Ndugulile amesema wizara yake inakwenda kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali za sektahiyo.

“Tunaenda kupitia sheria na kanuni zetu na tutafanya mabadiliko ili kukidhi mazingira ya sasa, tunakusudia kutunga sheria ya faraghana kulinda taarifa za mtumiaji (Data Privacy and Protection), nimekuwa msikilizaji wa mdahalo kwa kweli tumepata mengi kutoka kwa wadau na kama Serikali tunaenda kuyafanyia kazi kwa haraka” Ndugulile

“Muda wowote wadau leteni mawazo, maoni na ushauri ni namna gani tuboreshe na tusonge mbele uzuri hata mitandaoni nipo ukienda Twitter utanipata, Instagram nipo na uzuri kwa sasa inapatikana vizuri na mnaipata vizuri pia, kuhusu TCRA nimetoa maelekezo tayari wasifanye kazi kama Polisi bali kama mlezi, mimi sio muumini wa faini kubwa kubwa lazima tubadilike na tumeanza kubadilika, Ndugulile

Akizungumza kwenye mkutano huo  Dkt. Bello Moussa, Mkuu wa Ubunifu na Mikakatiya TEHAMA Huawei Kusini mwa Afrika amesema: “Mapinduzi ya Nne ya Viwandayanakuja na maendeleo ya kiteknolojia yanaendesha maendeleo ya ulimwengu, ni wakati mzuri sasa kwa Tanzania kutosalia nyuma, bali kuungana na ulimwengu wote kwa kufanya kazi kwenye maeneo ambayo yataharakisha Mapinduzi ya Nne ya Viwanda Tanzania katika Miaka 5 ijayo ”

Alitaja maeneo  hayo ambayo ni pamoja na mpango wa kitaifa wa TEHAMA kwa uchumi wa kidigiti, mkongo wa taifa wenye kasi  zaidi, ufikiwaji wa huduma ya internet maeneo ya vijijini na wataalamu wa wataalam wa TEHAMA.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC),Dk. Godwill Wanga amesema Tehama imeleta matokeo chanya katika sekta mbalimbaliikiwamo kupunguza gharama za uzalishaji, kuongezeka uwekezaji na ukuaji wauchumi wa nchi.

Post a Comment

0 Comments