Waumini wa dini ya Kiislam washauriwa kutoa misaada katika kipingi cha mwezi mtukufu wa Ramadhan

 


Na Maridhia Ngemela

Waumini wa dini ya Kiislam mkoani Mwanza wameshauriwa kutoa misaada mbalimbali katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan ikiwa ni moja wapo ya ibada na kuwakumbuka watoto yatima na wasiojiweza ili kuchuma swawabu kwa mwenyeziMungu.

Wito huo umetolewa na Sheikh wa mskiti wa Ibadh uliopo jijini hapa, Nouh Mousa wakati alipotembelea kituo cha Sos Children's Village Mwanza  kilichopo jijini hapa wilayani Nyamagana kinachotoa malezi na makuzi kwa watoto yatima kutoka  maeneo mbalimbali mkoani hapa.

Mousa alisema ni vema wananchi kuweka utaratibu wa  kutoa sadaka kwa watoto hao ambao wamepoteza wazazi wao  ili kuweza kuwapa faraja na wajione ni wenye kupendwa hapa duniani.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Shabab Daawat Islamiya, Ally Mbarak  alisema lengo la kutembelea  kituo hicho ni kuwatia moyo walezi ambao wanalea watoto hao  ili waweze  kutambua kuwa jamii inawathamini na kuwajali kwa kuona umuhimu wao.

"Tumekuja kuwapa moyo watoto hawa na walezi wao kwani ni jambo jema  kumthamini mtu  mwema ambaye anajali yatima  hata mtume amesema  atakuwa karibu na mja ambaye atakuwa  karibu na  atakaye  msaidia  mtoto yatima",alisema Mbarak.

Tumetoa sadaka yenye thamani ya sh milion 1  vitume nunua vitu mbalimbali ukiwamo unga wa ngano, mafuta ya kupikia, chumvi, Sabuni, Mchele, sabuni za unga mifuko miwili, maharage, Sukari mifuko miwili tunaamini vitawasaidia kwa kipindi hiki na tunawaomba watu wengine watembelee kotio hiki.

Naye  child and Youth Development officer, Masoud Hussein alisema  kituo hicho kina watoto 85 wakiwemo wakike 37 na wakiume 48  na kina watoto wa umri wa miaka miwili hadi 15.

"Sisi tunafanya kazi na Serikali na watoto wao tunawapokea  kutoka kwenye ofisi ya Ustawi wa jamii wanawafatilia kwa kina  wapojilidhisha wanasifa za kuwaleta kwenye kituo chetu wanawaleta na sisi tunawapokea", alisema Husein.

Kwa upande wake kiongozi wa wanawake wa kituo hicho Apoche  Mwenjesha  aliwashrukuru viongozi hao kwa kuona umuhimu wa kuwatembelea watoto hao ambao ni yatima kwani kutoa si utajili bali ni moyo wenye kuamini na kujali.

Post a Comment

0 Comments