Jun 18, 2021

Kama mwataka amani sawa mkitaka vita basi niko tayari-Kim Jong-un aiambia Marekani

  Muungwana Blog 3       Jun 18, 2021


Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema nchi yake inahitaji kujiandaa kwa "mazungumzo na makabiliano" na Marekani na "haswa kujiandaa kikamilifu kwa mapambano".

Bwana Kim alisema wanahitaji "haswa kujiandaa kikamilifu kwa mapambano ili kulinda hadhi ya serikali yetu na masilahi yake kwa maendeleo huru", na vile vile kuhakikisha mazingira ya amani na usalama wa Korea Kaskazini, kulingana na chombo cha habari cha serikali KCNA.

Alisema pia Korea Kaskazini "kwa kasi na mara moja" itashughulikia maendeleo yoyote na "kuzingatia juhudi za kudhibiti hali kwa rasi ya Korea".

Maoni yake ya hivi karibuni yanakuja siku chache baada ya Bw Kim kukiri rasmi kwamba Korea Kaskazini inakabiliwa na wasiwasi juu ya upungufu wa chakula.

Kabla ya uchaguzi wa Marekani , Bwana Biden alikuwa amemwita Bw Kim "jambazi", na siku chache kabla ya kuapishwa kwa Bw Biden, Korea Kaskazini ilijitokeza kwa onyesho la nguvu na gwaride kubwa la jeshi ambalo lilionyesha kombora jipya.

Mnamo Aprili Bw Biden aliitaja Korea Kaskazini kama "tishio kubwa" kwa usalama wa ulimwengu, na kusababisha jibu la hasira kutoka Korea Kaskazini ambayo ilisema taarifa hiyo ilidhihirisha dhamira ya Bwana Biden "kuendelea kutekeleza sera ya uhasama" kuelekea nchi hiyo.

Washington pia hivi majuzi ilikamilisha ukaguzi wa sera yake ya Korea Kaskazini na kusema kuwa Marekani itaendelea kulenga hatimae uharibifu kamili wa nyuklia katika peninsula ya Korea.

Bwana Biden ameahidi mbinu iliyowekwa na diplomasia na "uzuiaji mkali".

Msemaji wa Ikulu Jen Psaki alisema kuwa "sera yetu haitalenga kufikia makubaliano makubwa, na haitategemea uvumilivu wa kimkakati".

Marekani badala yake ingefuata "njia iliyosawazishwa ambayo iko wazi na itachunguza diplomasia na" Korea Kaskazini, alisema, akiongeza kuwa itazingatia kufanya "maendeleo ya vitendo".

Bwana Kim hapo awali alikuwa amekutana na mtangulizi wa Bw Biden, Donald Trump mara tatu, lakini mazungumzo juu ya uharibifu wa nyuklia mwishowe yalikwama.

"Utawala wa Biden umesema mpira uko mikononi mwa Korea Kaskazini, lakini utawala wa Kim umekuwa ukitumikia uvumilivu wa kimkakati," alisema Leif-Eric Easley, profesa mshirika wa masomo ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Ewha Womans huko Seoul.

"Inabakia kulenga maswala ya ndani na inataka kuona motisha kubwa kutoka Washington," ameongeza.

"Pyongyang inaweza kurudi kwenye mazungumzo tu baada ya kuonyesha nguvu na kufufua uchumi baada ya janga na majaribio ya kijeshi yanayozua uchochezi'

logoblog

Thanks for reading Kama mwataka amani sawa mkitaka vita basi niko tayari-Kim Jong-un aiambia Marekani

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment