Mbunge viti maalum asimulia alivyomkimbia mumewake baada ya kugombea uongozi


Na Maridhia Ngemela, Mwanza.

Wanawake wameshauriwa kutokimbia changamoto wanazokutana nazo katika nafasi walizonazo na wanazktegemea kugombea.

Hayo yamesemwa na baadhi ya wanaweke Mkoani Mwanza wakati wa semina ya kuongeza uwezo kwa wanawake walio viongozi na vijana wanaharakati na  wanaotarajia kugombea 

uongozi kwa nafasi mbalimbali hapa nchini ambayo imeandaliwa na mashirika binafisi, Femnet, Idea, wwp na Sweden Severige kwa kwa kuongozwa na Young and alive kwa kusimamiwa na Tamwa pamoja na   viongozu wabunge wanawake kwa  lengo la kuwapa uelewa wa kuwa kiongozi bora.

Mbunge viti maalum mkoa wa Mara Ghati Chomete ameelezea baadhi ya changamoto alizokutana nazo kipindi alipokuwa anagombea nafasi ya uongozi, amesema  hakupata mshikamano kutoka kwenye familia yake hususani mumewake ambae alimpinga vikali ameongeza kuwa   baadhi ya familia hawakubali kuongozwa na mwanamke kutokana na mila ambazo ni kandamizi katika jamii.

Chomete amesema alikutana na vikwazo mbalimbali ila hakuvunjika moyo kutokana na malengo aliyokuwa nayo ya kuwasaidia wanawake ambao walikuwa wanauhitaji katika jamii, amewasihi wanawake kutokubali kukatishwa tamaa na baadhi ya watu ambao hawakotayali kuona mchango wa mwanamke kwenye jamii.

Naye katibu wa chama cha walemavu (chawata) Jane Maira amesema kuwa kwa upande wa walemavu wanatamani sana kupata uongozi ila wanakutana na changamoto mbalimbali zikiwemo, miundombinu ya barabara, rushwa na kusababisha kutofikia malengo yao ambayo yanawakwamisha na kuwakatisha tamaa ya kuwa viongozi hapo baadae.

Maira amewashauri wanawake walemavu kutorudi nyuma bali wapambane katika nafasi walizomo na waweze kufanya mazuri zaidi ilikuiaminisha jamii kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi bora na wakuigwa.

Kwaupande wake mkurugenzi kutoka Tamwa Rose Reuben amesema , kwa muda mrefu wanawake tumekuwa nyuma kutokana na changamoto tunazokutana nazo kama, mila kandamizi, ukatili wa jinsia, kuolewa katika umri mdogo, kurithiwa kwenye ndoa kutokana na mila kandamizi.

Reuben amewashauri wanawake kujitambua na kufahamu nini ambacho wanachohitaji katika kutimiza ndoto zao na nimuhimu kujijenga kiuchumi ilikuwawezesha katika kipindi cha mapambano ya kutafuta uongozi.

 

Post a Comment

0 Comments