Pande katika majadiliano ya kufufua mkataba wa nyuklia wa Iran kukutana Jumapili


Pande zinazoshiriki mazungumzo ya kufufua mkataba wa nyuklia wa Iran zinatarajiwa kufanya mkutano rasmi leo mjini Vienna. 


Hayo yamesemwa na Umoja wa Ulaya.Iran na nchi nyingine sita zenye nguvu zaidi duniani zimekuwa zikijadiliana mjini Vienna tangu mwezi Aprili, kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa na Iran na Marekani.


Mkutano wa leo unajiri zaidi ya wiki moja baada ya duru hii ya mazungumzo kurejelewa tena na ni ishara kwamba kuna uwezekano wa mazungumzo hayo kuahirishwa.Wiki iliyopita, maafisa walidokeza kwamba tofauti bado zipo katika masuala muhimu.Marekani ilijiondoa kwenye mkataba huo mwaka 2018.

Post a Comment

0 Comments