Rais Biden na Waziri Mkuu wa Uingereza wanakutana kwa mara ya Kwanza

 


Rais Joe Biden wa Marekani na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson watafanya mkutano wa ana kwa ana unaolenga kupatikana kwa misingi mipya ya makubaliano, pamoja na athari za hatua ya Uingereza kujiondowa Umoja wa Ulaya.

Katika ziara yake hiyo ya kwanza ya nje ya Marekani tangu aingie maradarakani Biden na waziri mkuu huyo wa Uingereza wanategemewa kukubaliana juu ya muundo mpya wa makubaliano ya 1941 yaliyosainiwa na Winston Churchill na Franklin D. Roosevelt, ambao uliweka malengo ya baada ya Vita vya Pili vya Dunia kwa ajili ya demokrasia, biashara na fursa. 

Baada ya mazungimzo hayo ya pamoja Johnson na Biden watajumuika katika mkutano wa kundi la mataifa saba yenye nguvu kiuchumi la G7 kuanzia Ijumaa hadi Jumapili, ambao pia utahudhuriwa viongozi wa Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Japan.

Post a Comment

0 Comments