Jun 11, 2021

Rais Kenyatta atoa ombi kwa watengenezaji silaha haramu

  Muungwana Blog 2       Jun 11, 2021

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa ombi kwa watengenezaji silaha haramu kujisalimisha na kufanya kazi katika kiwanda kipya cha silaha kilichoanzishwa.

Kulingana na taarifa za The Daily Nation, Kenyatta, alitoa hotuba yake wakati wa uharibifu wa silaha haramu zilizokamatwa katika mkoa wa Kajiado nchini humo, ambapo aliahidi msamaha kwa watengenezaji silaha haramu ikiwa watajisalimisha.

Akibainisha kuwa silaha ambazo hazijasajiliwa zilizokamatwa Kenya zilizalishwa ndani ya nchi, Kenyatta alisema kuwa watengenezaji wa silaha wanaweza kuacha kazi na kufanya kazi katika kiwanda cha silaha kilichoanzishwa hivi karibuni kwa kuzingatia uzoefu wao.

"Nataka kutoa pendekezo leo. Kenya sasa inaweza kutengeneza silaha zake ndogo ndogo, na nyinyi ambao mnajishughulisha kutengeneza kwa wahalifu, nawaomba tuwape kazi ya kudumu ya kutengeneza silaha halali. Mtasaidia uchumi wetu kukua."Alitoa taarifa hiyo.

Kenya iliunda kiwanda kipya cha silaha mwezi Aprili kwa gharama za takriban dola milioni 36.

 

logoblog

Thanks for reading Rais Kenyatta atoa ombi kwa watengenezaji silaha haramu

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment