RUNALI chauza tani 3,595 za ufuta, mwenyekiti awapa neno watendaji na viongozi wa AMCOS



Na Ahmad Mmow, Ruangwa. 

Chama kikuu cha ushirika cha RUNALI kilichopo mkoani Lindi, leo kifanikiwa kuuza tani 3,395 na kilo 391 za ufuta zilizo katika maghala makuu ya Umoja, Export na Lipande. 

Kwamujibu wa kaimu mraji msaidizi wa ushirika wa mkoa wa Lindi, Richard Zengo katika mnada huo wa pili kwa RUNALI na wasita kwa mkoa wa Lindi,  bei ya juu ni shilingi 2,333 na bei ya chini ni shilingi 3,313. 

Kampuni zilizofanikiwa kununua ufuta huo uliopo katika maghala ya Umoja(Liwale), Lipande (Ruangwa) na Export(Nachingwea) ni Export Trading, Solartes Mega Company Ltd, Lenic Tanzania Ltd, Afrisian Gining Ltd,Iniciator, Dizgotic Ba Company Ltd na S.M Holding Ltd. 

Nyingine ni Tanzania China International Company Ltd na HS Impex Ltd. Ambapo ghala la Umoja lina tani 722 na kilo 458, ghala la Export lina tani 1,431 na kilo 882 na ghala la Export tani 1,241 na kilo 51. 

Aidha katika ghala la Umoja ufuta huo umenunuliwa kwa bei ya juu shilingi 2,323 na bei ya chini ni shilingi 2,313 kila kilo moja, ghala la Lipande bei ya juu shilingi 2,326 na bei ya chini shilingi 2,315 kila kilo moja na katika ghala la Export bei ya juu ni shilingi 2,333 na bei ya chini shilingi 2,323 kila kilo moja. 

Akizungumza baada ya wakulima kukubali kuuza ufuta huo kwa bei hizo, mwenyekiti wa RUNALI, Audax Audax Mpunga aliwaasa wakulima kuendelea kulinda ubora wa ufuta ili bei ziendelee kupanda. Kwani thamani ya mazao inaanzia katika ngazi awali ambayo ni wakulima. 

Mpunga aliwataka viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) wahakikishe taarifa za wakulima zinatumwa haraka katika maeneo yanayositahili kutumwa ili wakulima walipwe kwawakati. 

Mpunga ambae alisema hana mashaka na watendaji wa RUNALI aliweka wazi kwamba kuchelewesha malipo ya wakulima kutachangia wanafunzi washindwe kupata mahitaji muhimu. Lakini pia wakulima hao watashindwa kupapalia mashamba ya mikorosho. 

'' Wanauhitaji mkubwa wa fedha hizo. Kipindi hiki cha likizo wanataka wanunue vifaa vya shule vya watoto wao, lakini pia fedha hizo watumie kuwalipa vibarua wanaopalilia mikorosho yao. Hakikini taarifa na kupeleka kwa wakati ili malipo yafanye kabla ya mnada unaofuata,'' alisema Mpunga. 

Mnada wa leo ambao umefanyika mjini Ruangwa ni wapili kwa chama kikuu cha RUNALI na mnada wa sita kwa mkoa wa Lindi kwa msimu wa 2021. Ambapo chama cha Lindi Mwambao tayari kimefanikiwa kufanya minada minne. 

Post a Comment

0 Comments