Jun 11, 2021

RwandaAir yasitisha kwa muda safari zake Uganda

  Muungwana Blog 2       Jun 11, 2021

 


Shirika la ndege la Rwanda, RwandAir imetangaza kuwa imesitisha kwa muda safari zake za ndege za kwenda na kutoka kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Uganda wa Entebbe mara moja.

“Kutokana na kuongezeka kwavisa vyaCovid-19 nchiniUganda, RwandAir inatangaza kusitishwa kwa safari zake za ndege za kuelekea na kutokaEntebbe kuanzia tarehe 10 Juni 2021, hadi tangazo linguine litakapotolewa,” Taarifa ya kampuni hiyo ya ndege ya Rwanda ilisema.

Iliongeza kuwa : “RwandAir inaomba radhi kwa usumbufu uliosababishwa na hatua hiyo.”

Shirika hilo lilisema kuwa wateja waliothiriwa ‘’wanaweza kupanga upya safari na kusafiri baadaye, pale safari hizo zitakaporejeshwa tena–au waombe kurejeshewa pesa zao za nauli.”

Uganda imeshuhudia ongezeko la idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona, jambo lililowalazimisha maafisa kuweka sheria inayowataka watu kupunguza shughuli na matembezi yasiyo ya lazima kwa muda wawiki sita.

logoblog

Thanks for reading RwandaAir yasitisha kwa muda safari zake Uganda

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment