Serikali yaahidi kuilipa ATCL

 


Na Farida Saidy, Morogoro. 

Serikali imeahidi kulipa madeni yote wanayodiwa na shirika la ndege Tanzania  ili kuhakikisha shirika hilo linajikwamua kiuchumu na tayari mikakati ya ufnikisha hilo imeshapangwa ,huku ikiwatoa hofu watanzania kuwa shirika lipo imara na litaendelea kutoa huduma kwa wananchi.

Akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo mjini Morogoro,amesema maamuzi hayo ya Serikali yatalifanya shirika hilo kujiendesha kwa faida na kuleta tija kwa wafanyabishara  wa ndani na njee ya nchi wanaotegemea usafiri wa unga.

Aidha amesema  Serikali itaendelea kuweka fedha katika shirika hilo ili   kuboresha ufanisi na utendaji kazi utakaosaidia kukuza usafiri wa anga nchini na kuwavutia wasafiri kutokana na huduma mbalimbali zinazoendelea  kutolewa .

Katika hatua nyingine amesema serikali kupia ATCL haitamfumbia macho wakala yeyote atakaye ficha mawasiliano ya mteja atakaye muhudumia,kwani kufanya hivyo ni kumnyima haki mteja ya kupata taarifa muhimu kutoka kwenye shirika jambo ambalo hutaleta usumbufu kwa wateja pale panapotokea kusitishwa au kubadilishwa muda wa safari.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa  shirika la ndege Ladislaus Matindi ATCL ameeleza  mikakati ya kuboresha huduma za usafiri katika maeneo mablimbali ya ndani na nje ya nchi.

Aidha ameongeza kuwa pamoja na changamoto ya ugonjwa wa korona  shirika litaendelea kujiimarisha kwa kutoa huduma zilizo bora na kuzingatia viwango  vilivyowekwa kimataifa.


Post a Comment

0 Comments