Jun 11, 2021

SHIVYAWATA Mkoa wa Manyara yapata Viongozi wapya

  Muungwana Blog 2       Jun 11, 2021


Na John Walter-Manyara.

Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu (SHIVYAWATA) mkoa wa Manyara baada ya miaka zaidi ya kumi , hatimaye wamepata uongozi mpya utakaosimamia na kutatua changamoto zote zinazowakabili kwa muda wa miaka mitano.

Uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa mkoa Manyara, ulisimamiwa na Maafisa ustawi wa Jamii Anna Obedi na Jackline Goodluck ambapo wamewataka viongozi hao wapya kuunganisha vyama vyote vya watu wenye ulemavu na kuelewana.


Viongozi waliochaguliwa ni mwenyekiti Sara Shabani kutoka wilaya ya Hanang, Katibu Anna Ngalawa kutoka Babati na Mweka hazina Suzana Mushi kutoka Babati.

 

logoblog

Thanks for reading SHIVYAWATA Mkoa wa Manyara yapata Viongozi wapya

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment