Wananchi fuatilieni vyeti vya kuzaliwa ni muhimu

 


Na Maridhia Ngemela Mwanza.

Wananchi wameshauriwa kufahamu umuhimu wa kuwa na cheti cha kuzaliwa ilikuondokana na usumbufu unaoweza kujitokeza pindi kinapohitajika.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Robery

Luhumbi amezitaka halmashauri zote Mkoani hapa  kwenda kuiga na kujifunza  mbinu walizotumia  halmashauri ya Misungwi  kwa utekelezaji wa usajili wa watoto na  utoaji wa vyeti kwa kiwango cha juu.


Hayo aliyasema leo kwenye kikao cha hamasa na tathimini ya Mpango wa usajili wa watoto chini ya umri wa miaka mitano alisema halmashauri hiyo  imefanya vizuri kwenye zoezi hilo ni vema viongozi wa  halmashauri nyingine kujifunza kutoka kwao.


 "Halmashauri hii  tupo kwenye mkoa mmoja na wamefanikiwa  kwanini  wengine wa shingwe wakati changomoto zinafanana tumieni mafanikio yao kama fursa kwenu ili muweze kufikia malengo",alisema Luhumbi. 


Naye Mkuu wa Wilaya ya Halmashauri ya Misungwi,Juma Sweda alisema walianzisha kampeni kwa kila katibu talafa kuwapeleka wananchi kwenye Kata kwa ajili ya  kusajili watoto  wenye umri wa chini ya miaka mitano kwa ajili ya kuwapa vyeti vya kuzaliwa


Alisema rita imekuwa msaada mkubwa kwao na kupelekea kufanikiwa kwenye zoezi hilo kwani wananchi walikuwa wanatumia gharama kubwa kwa ajili ya kufata huduma hiyo ya kufatilia cheti ilikuwa kubwa ndo maana wakaona wawafuate wananchii kwani walikuwa wanatoka umbali wa km 100 ili kuwarahisishia gharama za upatikanaji wa cheti cha kuzaliwa 


"Lengo letu ni kuhakikisha tunasajili watoto kwa asilimia 100 kwani Sasa hivi tumeweka utaratibu wa  mtoto anapozaliwa tu apate cheti cha kuzaliwa au baada ya wiki moja tangu alipozaliwa  awe amepata  huduma hii ili kuweza kupunguza usumbufu utakaweza kujitokeza pindi anapoenda kuandikishwa Shule,"aliaema Sweda.


Naye  Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufisi na Udhamini (RITA) Emmy Hudson ameimba serikali imeondoa gharama za ufatiliaji wa huduma ya upatikanaji wa cheti cha kuzaliwa pamoja na ada kwa kushirikiana  na wadau ili mwananchi aweze kupata huduma hiyo bila malipo.


Alisema   mfumo huo umeleta mageuzi  ya kutumia teknolojia katika kusafilisha kumbukumbu za walio sajiliwa na kuzitunza  kwenye kanzi data ya Rita.


Alisema  tangu Mpango huo ulipoanza mwaka 2013  mpaka sasa wametekeleza kwenye 20 ya Tanzania bara wamesajili na kutoa vyeti kwa watoto milioni 5.


9 kwa mikoa miwili, Mbeya na Mwanza mpaka mwaka jana halii imesaidia  kuongeza kiwango cha Watoto cha walisajiliwa kutoka asilimia 13 mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 55 mwaka 2020.


"Utekelezaji wa mpango  huu wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika Mkoa wa Mwanza ulianza mwaka 2015 kwani ulikuwa  Mkoa wa pili kuanza zoezi hili usajili ulifanyika kwenye vituo vya tiba tu tofauti na mikao mingine huduma zinapatikana kwenye ofisi za Watendaji wa Kata.


"Kwa mujibu wa takwimu hali ya Mkoa wa Mwanza hairulidhishi kwani mpaka Sasa ni asilimia 29.4  ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano  wamepata vyeti vya kuzaliwa hii ikimaanisha usajili kwenye vituo hufabyika Kwa kiwango kidogo na taarifa za wanaofanyiwa zoezi hili haziingi kwenye simu.


"Sababu  za kiwango cha usajili kushuka Mkoa hapa ni kuondoka Kwa wasajili wasajili wasaidizi kuhama vituo, kubadilishiwa majukumu na kutokupewapo mfumo mahususi wa kukabidhi majukumu Kwa anayekabidhiwa ofisi alisema  Emmy.


Kwa upande wake Kaimu Meneja wa wakala wa usajili ufilisi na udhamini  (RITA) Patricia Mpuya alisema utekelezaji wa Mpango huo cheti kinachotolewa kwa mtoto ni toleo la kwanza.


"Cheti hiki hujazwa kwa mkono na ni halali kwa matumizi yoyote kwani anaposajiliwa hupewa namba maalum ya utambulisho ambayo hupatikana kwenye vyeti vilivyochapwa kwa mashine," alisema Patricia.


Aidha akichangia mada kwenye kikao hicho Mwenyekiti wa  Halmashauri ya Wilaya ya Magu,Mpandalume Simon alisema ni vema zoezi hilo kuwashirikisha wanasiasa, Watendaji wa  vijiji,   viitongoji, wasanii na wananchi tofauti na watendaji wa kata.

Post a Comment

0 Comments