Na Amiri Kilagalila,Njombe
Edita
Mangita (40) mkazi wa mtaa wa Matema kata ya Maguvani mjini Makambako
amefariki dunia baada ya kujifungia na jiko la mkaa Katika kibanda chake
cha biasahara.
Kwa
mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema tukio
hilo limetokea Julai 28,2021 ambapo marehemu Editha aliamua kubaki na
kulala katika kibada chake cha biashara Ili kuwahi wateja wake wa
asubuhi.
Aidha kamanda
Issa amewataka wananchi wa mkoa wa Njombe kuacha kulala na majiko ya
mkaa ndani huku akitoa wito kwa wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu
kuhusu madhara hayo Ili kuiokoa jamii.
Hivi
karibuni mjini Njombe kulitokea kifo cha watu wawili wapenzi baada ya
kulala na jiko la mkaa ili kupunguza baridi katika chumba chao.
Kamanda
Issa ametaja tukio lingine la mwanamke mmoja Imelda Mgeni ametelekeza
mtoto mwenye umri wa miezi mitatu kwa mume wake naye kwenda
kusikojulikana.
0 Comments