Jul 21, 2021

Merkel kudihinisha msaada kwa waathirika wa mafuriko

  Muungwana Blog       Jul 21, 2021

 


Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel leo anakutana na baraza la mawaziri kwa ajili ya kuidhinisha msaada wa dharura wa kuyajenga upya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko nchini humo. 


Shirika la habari la Ujerumani, DPA limeripoti kuwa msaada wa awali unatarajiwa kuwa euro milioni 400, huku nusu ya fedha hizo zikitolewa na serikali ya shirikisho na zilizobaki zimetolewa na serikali za majimbo. Baadae msaada mkubwa wenye thamani ya mabilioni ya euro unatarajiwa kutolewa kwa ajili ya kujenga upya miundombinu muhimu kama vile barabara na reli. 


Ujerumani pia inafikiria kuomba msaada wa fedha kutoka kwenye Mfuko wa Mshikamano wa Umoja wa Ulaya. Wakati huo huo, Shirika la Usaidizi wa Kiufundi la Ujerumani, THW, limesema hakuna dalili ya kuwapata watu waliokwama kwenye vifusi wakiwa hai. Watu 169 wamekufa kutokana na mafuriko hayo yaliyotokea wiki iliyopita nchini Ujerumani

logoblog

Thanks for reading Merkel kudihinisha msaada kwa waathirika wa mafuriko

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment