Jul 21, 2021

Mwanamke aiba almasi ya mamilioni kwa kuibadilisha ''kijanja'' na mawe

  Muungwana Blog       Jul 21, 2021

 


Lulu Lakatos, mwenye miaka 60, anadaiwa kujifanya mtaalamu wa masuala ya tathimini ya vito vya thamani kutoka Boodles katikati mwa jiji la London.


Bi Lakatos alithaminisha mawe saba ya almasi katika mtaa wa New Bond kabla ya kuyaweka kwenye mkoba, hakimu alielezwa.


Lakini mkoba ulipofunguliwa, ndani yake kulikuwa na mawe madogo saba, mahakama ya Southwark Crown ilielezwa.


"Almasi ziliibiwa na mshtakiwa kwa njia za udanganyifu," mwendesha mashtaka Philip Stott alisema.


"Njama ambayo anayodaiwa kufanya ilikuwa moja wapo ya ustadi wa hali ya juu, upangaji, hatari, na tuzo."


Lakatos, aliyezaliwa Romania lakini Ufaransa, amekana kufanya njama za kuiba tarehe au kabla ya Machi tarehe 10 mwaka 2016.


Mahakama ilielezwa kuwa, mnamo Februari 2016, mwenyekiti wa Boodles Nicholas Wainwright alitambulishwa kwa mtu anayejiita "Simon Glas", ambaye alisema alikuwa na nia ya kununua almasi yenye thamani kubwa kama uwekezaji.


Wawili hao walikutana Monaco mwezi uliofuata, ambapo Bwana Wainwright alitambulishwa kwa mwenza wa Glas, Mrusi anayeitwa "Alexander", na uuzaji wa almasi saba zenye thamani kubwa ilikubaliwa baada ya mazungumzo zaidi.


Mawe hayo ya thamani ya pauni milioni 4.2m, yalihusisha umbo la moyo la almasi lenye thamani ya pauni milioni 2.2 na almasi ya karati tatu ya rangi ya pinki yenye thamani ya pauni mil 1.1.


Mthamini wa vito, "Anna", aliyeagizwa na wanunuzi alitakiwa kuchunguza mawe kabla ya kuwekwa kwenye mkoba uliofungwa litakaloshikiliwa na Boodles hadi vito vilipopokea fedha.


Bi Lakatos anadaiwa kujifanya Anna, mbapo alisindikizwa kwenda kwa sonara, na kusubiri kwenye chumba tarehe 10 mwezi Machi na Bwana Wainwright na mtaamu wa vito Emma Barton anayemiliki kampuni yake.


'Alibadili mikoba inayofanana'

Bwana Stott alisema Bi Lakatos alitaka kuchunguza na kuthamini almasi saba kabla ya kuzifunga kwenye karatasi ya tishu iliyokatwa na kuiweka ndani ya visanduku visivyoonesha ndani


''Uchunguzi ulipokamilika , visanduku hivyo viliwekwa mikoba yenye zipu, kisha kufungwa na kufuli,''Jaji wa mahakama alielezwa.


Waendesha mashtaka walisema Bi Lakatos aliweka mkoba huo uliofunwa kwenye mkoba wake wa mkononi wakati Bw. Wainwright alipopanda ngazi kwenda juu.


''Inaonesha mkoba huo ulibadilishwa na mwingine unaofanana nao,'' Bw. Stott alisema.


Bw. Scott anasema Bi Lakatos alienda kubadili nguo zake kwenye maliwato ya mgahawa na kuvaa koti jeusi badala ya alilovalia awali, akishirikiana na mtu mwingine.


Kisha alitumia pasi yake mwenyewe kuondoka jijini London.Mahakama ilielezwa.


Bi.Lakatos alikamatwa Ufaransa baada ya kutolewa hati ya kukamatwa ya Ulaya mwezi Septemba mwaka jana kabla ya kupelekwa Uingereza.

logoblog

Thanks for reading Mwanamke aiba almasi ya mamilioni kwa kuibadilisha ''kijanja'' na mawe

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment