Nicosia kuomba UN kufanya mkutano kuhusu kisiwa cha Cyprus


 Serikali ya Jamhuri ya Cyprus iliyoko mjini Nicosia inayotambulika kimataifa inataka kuliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufanya mkutano usio wa kawaida kuhusu kisiwa hicho kilichogawanyika. 


Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus, Nikos Christodoulides ameiambia redio ya taifa leo kuhusu hatua hiyo, wakati ambapo mvutano kuhusu kisiwa hicho cha Cyprus ukiongezeka. 


Jana, Cyprus Kaskazini inayotambuliwa na Uturuki ilisema itaendelea na mpango wake wa kuufungua mji wa Varosha ambao ulitelekezwa tangu vita vya 1974 ambavyo vilikigawa kisiwa katika pande mbili. 


Cyprus imegawanyika kati ya Cyprus ya upande wa Uturuki ambayo ni ya kaskazini na Cyprus ya upande wa Ugiriki ambayo ni kusini tangu vita vya mwaka 1974 baada ya mapinduzi ya Ugiriki na jeshi la Uturuki kuingilia kati. 


Jamhuri ya Cyprus ya Uturuki inatambuliwa tu na Uturuki, huku Cyprus ya Ugiriki iliyoko Kusini ikiwa inatambuliwa na Umoja wa Ulaya tangu mwaka 2004.

Post a Comment

0 Comments