Njia rahisi ya kupata wazo la biashara


Upo usemi usemao wenye mawazo ya biashara wengi hawana pesa, na wenye pesa nao hawana mawazo ya biashara. Hili lipo wazi kila kona si rahisi kupata wazo la biashara kama vile uzaniavyo, hii ikiwa na biashara nyingi zinazoanzishwa leo nying hazidumu kwa sababu waanzisha biashara hizo huwa hawaichui biashara hiyo kwa kina kabla ya kuianzisha.

Biashara nyingi huanzishwa kila mwaka ila huwa hazidumu zaidi ya miaka miwili. Kupata wazo la biashara itakayodumu na kufanikiwa ni msingi wa kuanzisha biashara / kampuni.

Zifutazo ndizo njia zitazokusaidia kuanzisha biashara zenye mafanikio:

Kwanza jifunze kutambua fursa. Biashara ni fursa, angalia matatizo mbalimbali yanayowazunguka  watu na namna gani bora ya kuyatatua na ukapata faida. Fursa inayodumu inatokana na kupata njia bora ya kutatua matatizo ya msingi ya watu wanaokuzunguka.

Andika matatizo yote unayodhani yanahitaji utatuzi wa kudumu unayoweza kuyatatua. Andika kadiri unavyokutana nayo. Pia unaweza kuangalia upungufu katika soko la bidhaa au huduma ukaandika upungufu huo unaoweza kuutatua. Hata katika kazi unayofanya inawezekana kuna fursa fulani iliyojificha kama tatizo, hatua ya kwanza ni kuandika yote.

Pili fikiria suluhisho la mapungufu/matatizo hayo. Pitia list yako ya matatizo na mapungufu na uanze kufikiria suluhisho la moja baada ya jingine. Mengine unaweza kukuta suluhisho lipo ila limeelemea upande mmoja nawe unaweza kutatua kwa namna nyingine. Mfano kuna maduka ya nguo ila hakuna la nguo za watoto pekee ukatumia hiyo fursa. Suluhisho lazima liwe kweli linatatua tatizo lililopo na kwa ubora wa hali ya juu na linakupa faida.

Unawezakuta matatizo kadhaa unaweza kuyatatua, ili biashara iwe ya kudumu chagua lile ambalo linakuvutia, unaona kabisa ndio uwezo wako upo huko na unalipenda. Ukifanya kitu unakipenda utakuwa tayari kukabiliana na changamoto zote utakazokutana nazo.

Zipitie kwa uangalifu, fanya utafiti wa kutosha kisha chagua utakayoifanyia kazi. Usianze na fursa nyingi kwa wakati mmoja utakosa umakini(focus). Anza na moja hadi imesimama ndio utafute nyingine.

Post a Comment

0 Comments