Uingereza inatarajia Ulaya kuzingatia pendekezo lake

 Uingereza imesema inatarajia Umoja wa Ulaya utachukua muda wake kuzingatia pendekezo la Uingereza kwa ajili ya kubadilisha sehemu ya makubaliano ya Brexit yanayohusu Ireland Kaskazini. 


Hayo yameelezwa leo na msemaji wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson. Amewaambia waandishi habari kwamba Uingereza imekuwa ikisema mara kwa mara kwamba namna ambavyo itifaki inatumiwa haikubaliki na inahitaji kushughulikiwa haraka. 


Anasema anatarajia Umoja wa Ulaya utalizingatia pendekezo na maoni yao na kutoa majibu yanayofikirika. Wakati huo huo, Ireland imesema iko tayari kubadilika na kuwa wabunifu kuhusu Itifaki ya Ireland Kaskazini, lakini haitaki kujadili tena mkataba wa Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya. 


Naibu Waziri wa Ireland anayehusika na masuala ya Ulaya, Thomas Byrne amekiambia kituo cha televisheni cha Sky kwamba kuna uwezakano wa kubadilika, lakini hawataki kujadiliana tena kuhusu itifaki.

Post a Comment

0 Comments