Jul 21, 2021

Wiki ya Taasisi ya PASS Trust kuanza kesho Jijini Dodoma fulsa kwa wakulima, Wafugaji na wajasiliamali

  Muungwana Blog       Jul 21, 2021


Taasisi ya PASS Trust imeandaa wiki ya maonyesho ya wakulima, wafugaji na wajasiliamali kujadili changamoto zao na namna ya kujikwamua walipo huku Mkuu wa  Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimwer akiihimiza taasisi ya utafiti wa Kilimo nchini (TARI) kushirikiana na taasisi ya PASS Trust inayojihusisha na masuala ya kilimo ili kuendeleza Kilimo cha Zabibu jijini Dodoma.


Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Dodoma Antony Mtaka,Mkuu wa Wilaya Shekimwer  amesema kilimo cha zabibu ni zao ambalo endelevu na ukianza kulima utaendelea kuvuna ndani ya miaka 50,hivyo nivema taasisi hizo zikatengeneza wataalamu kwa ajili kuinua kilimo hicho kiwe na tija.


Shekimwer amesema Serikali imeweka mkazo katika suala la Kilimo hususani katika zao la zabibu,hivyo TARI wanapaswa kushirikiana na Pass katika kuhakiisha wanasaidiana kuinua sekta ya kilimo mkoani hapa.


“Hivi karibuni Waziri Mkuu alisisitiza zao la zabibu litilwe mkazo,hivyo nao wanapaswa kushikana na PASS TRUST kuinua kilimo cha zabibu mkoani hapa,” amesema Shekimwer.


Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Trust Pass Anna Shanalingigwa amesema Pass Trust imedhamini miradi 46,300 huku wajasiriamali mil 1.7 wamenufaika na udhamini huo.


Mbali na hilo amebainisha kuwa na taasisi hiyo ya Pass ni kutoka sekta ndogo za Mifugo,uzalishaji wa mazao,Viwanda vya usindikaji,biashara ya mazao,mitambo ya mashine za viwanda,Miundombinu bora ya umwagiliaji,usafirishaji wa mazao ya kilio,Ufugaji Nyuki,Ufugaji Samaki na biashara ya pembejeo.


Kaimu Mkurugenzi huyo amesema lengo lao ni kuona wajasirimalai wanafanya ujasiriamali wenye tija kupitia taasisi ya Pass Trust.


Katika hatua nyingine Shanalingigwa amesema wanazindua kampuni ya Pass Leasing yenye lengo la kutoa mikopo ya zana za kilimo kwa ajili ya wajasiriamali kujiinua kiuchumi.


Amebainisha kuwa  kampuni hiyo itawawezesha wakulima  wadogo wa kati na wakubwa ikiwemo vikundi vinavyojihusisha na shughuli za kilimo katika mnyonyoro mzima wa thamani kunufaika na zana ambazo zitatolewa kwa mkopo.


Kutokana na hilo amesema wajasirimalai wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika wiki ya Pass ambayo inatarajia kuanza kesho July 22 hadi Julai 24 jijini Dodoma amebainisha wajasirimalai wanapaswa kuchangamkia fursa ambayo ni muhimu kwao kwa ajili ya kujiendeleza na kilimo pamoja na ufugaji.


logoblog

Thanks for reading Wiki ya Taasisi ya PASS Trust kuanza kesho Jijini Dodoma fulsa kwa wakulima, Wafugaji na wajasiliamali

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment