Ticker

6/recent/ticker-posts

Idadi ya vifo vitokanavyo na corona vyafikia 100,000 Ujerumani

 


Ujerumani imetangaza rekodi mpya ya maambukizi ya virusi vya corona leo wakati vifo vitokanavyo na virusi hivyo vikipindukia 100,000 huku serikali mpya ijayo ikijitayarisha kukabiliana na makali ya wimbi la nne la janga la COVID 19. 


Awali Ujerumani ilikabiliana vyema na virusi hivyo kuliko taifa lengine lolote barani ulaya lakini kwa sasa maambukizi yameongezeka mno nchini humo huku vyumba vya wagonjwa mahututi vikikaribia kujaa. 


Watu 351 wamekufa ndani ya saa 24 na kuifanya idadi ya waliokufa kufikia 100,119 hii ikiwa ni kulingana na taasisi ya magonjwa ya kuambukiza ya Ujerumani ya Robert Koch (RKI). 


Mgogoro wa afya unazodi kutanuka kutokana na ugonjwa wa COVID 19 nchini Ujerumani unatoa changamoto kubwa kwa serikali mpya ya muungano inayotarajiwa kuchukua usukani kutoka kwa Angela Merkel mwezi Ujao.

Post a Comment

0 Comments