Israel yaonesha mashaka ya Iran kuondolewa vikwazo


Israel imeonesha wasiwasi mkubwa wa huenda mataifa makubwa yataiondolea Iran vikwazo kwa makubaliano yasiyo ya kuridhisha katika kuachana na mpango wake wa nyuklia.


Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa taifa hilo, Naftali Bennet, ikiwa kabla ya kuanza kwa mazungumzo mapya ya mzozo wa nishati ya Iran na mataifa makubwa kwa zingatio la makubaliano ya 2015.


Waziri Mkuu Bennett aliliambia baraza lake la mawaziri kupitia televisheni kwamba ujumbe huo wanauwasilisha kwa yeyote iwe kwa Marekani au kwa taifa lingine lolote linalofanya mazungumzo na Iran.


Kauli hiyo inatolewa wakati ambapo Mwanadiplomasia wa Iran, Mohammadreza Ghebi, akinukuliwa na shirika la habari la Iran, ISNA, kwamba timu ya Iran iliwasili mjini Vienna jana Jumamosi na kuanza mikutano katika ngazi ya wataalamu ambayo inahusisha viongozi wa timu za majadiliano za Urusi na China pamoja na mratibu wa Umoja wa Ulaya, Enrique Mora.

Post a Comment

0 Comments