Kanuni za kuikuza biashara ndogo ili iwe biashara kubwa

 


Kila kitu kinachoanza kwa hatua ndogo kinatakiwa kukua katika ukubwa, hivyo unapoonzisha biashara ndogo basi fahamu namna ambavyo biashara hiyo itakuwa kubwa.

Zifutazo ndizo kanuni za kuikuza biashara ndogo ili biashara kubwa.
Jitahidi pia kujua washindani wako wanafanya nini haswa wale ambao wako juu yako zaidi. Hii itakusaidia sana kuweza kujua ni mambo gani ambayo unaweza kuyatumia kwa nafasi yako kuweza kupanda juu zaidi ya hapo ulipo, usijifungie tuu ndani na wala usitake kujua wengine pia wanafanyaje kitu ambacho kinataka kufanana na chako. Fanya uchunguzi kwa kuingia google andika kitu ambacho unataka kujua kuhusu biashara yako na baada ya hapo andika pembeni mapungufu ambayo umeyaona katika biashara yako ambayo sasa unaweza anza kufanyia kazi pia.

Mitandao ya kijamii ni sehemu nzuri ya kuweza kutangaza biashara yako, hakikisha unaonekana kwamaana ya kufanya biashara sio unaonekana kwa manufaa ya watu kukuona na wewe upo kwenye mtandao. Kuna mitandao kama facebook, instagram, twitter, linkeldn inanguvu sana kwa wafanyabiashara haswa kuweza kutambulisha biashara yako kwa watu ambao huwajui pia.

Nimekuwa nikitumia mitandao hii katika shughuli zangu na nimeona matokeo makubwa sana kwa kipindi kifupi nawe inawezekana hebu tenga muda kwenye kujifunza kutumia mitandao ikufanyie biashara.

Weka malengo katika biashara yako. Bila malengo katika biashara yako unaweza kubaki hapo hapo ulipo. Hakikisha unapoanza biashara yako uweze malengo kwa kuangalia unataka biashara yako iweje baada ya muda flani na ufanye nini kwa wakati huo ili uweze kusogea katika kutimiza malengo yako hayo mfano umeanza biashara ya 100,000/= na katika malengo yako unataka baada ya mwaka mmoja biashara yako iwe ya mtaji wa 1,000,000/= hapa ni lazima upange kila siku ufanye nini kuweze kufanya ndoto yako kutimia, lakini pia ni lazima ujue mambo gani unatakiwa kuacha.

Ijue biashara yako na jiendeleze katika kujua mambo mapya ambayo yatakusaidia kuweza kuongeza ubunifu katika biashara yako ambayo unaifanya. Usilale na kuamka tuu na kwenda kwenye biashara yako jiulize leo umejifunza nini kipya cha kuongeza katika biashara yako na umegundua nini unatakiwa kupunguza ili uzidi kusonga mbele na biashara yako izidi kuwa mpya katika macho ya wateja wako. Ukiwani mtu wa kubaki vile vile katika biashara yako utakimbiwa na wateja na mwisho wa siku utaanza kuisema biashara yako ni mbaya. Kuna mambo kama kujua jinsia ya kuongoza mzunguko wa hela katika biashara yako, jinsi ya kumtawala mteja wako na kumfanya wa kudumu, kujua soko jipya kwaajili ya bidhaa yako n.k

Post a Comment

0 Comments