Nov 25, 2021

Mambo yatakayokusaidia kuwa Chanya katika maisha yako

  Muungwana Blog       Nov 25, 2021

 

Kuna vitu vikubwa viwili ambavyo kama utaamua kuvitumia vyema vinauwezo mkubwa sana wa kuweza kubadilisha maisha yako kwa kiwango cha hali juu sana. Na endapo utaamua kuvitumia vitu hivyo katika hali isiyofaa vina uwezo mkubwa pia wa kuweza kukutengenezea majuto katika maisha yako yote.

Vitu hivyo ni :

Kufanya Uchaguzi sahihi.

Kuna msemo unasema" kupanga ni kuchagua na kutenda ni kuamua" na hii ni siri kubwa iliyopo katika mafanikio yako. Unatakiwa kufanya tafakari makini juu ya kuchagua vitu muhimu vya kufanya katika maisha yako yote. Na kufanya uchaguzi wa mambo mbalimbali hakikisha ni mambo chanya.

Kwani maisha yetu yamekuwa hayana mtiririko ambao unaeleweka hii ni kutokana tumeshindwa kufanya uchaguzi sahihi wa mambo tunayoyataka.

Hivi hajawahi kutembelewa na ndugu, jamaa, au rafiki nyumbani kwako? Bila shaka umewahi, na je ulipomuuliza atatumia nini mgeni huyo kati ya juisi na maji , je alikujibu nini? Bila Shaka nafikiri alikwambia nitatumia chochote.

Majibu ya aina hii ndiyo ambayo yamesababisha maisha yetu kuwa magumu, wengi wetu tumekuwa hatujui ni nini ambacho tunachotaka, hali hiyo imepelekea kuwa tayari kufanya jambo lolote. Lakini ukweli ni kwamba maisha yako ili yawe bora ni lazima ujue ni kitu gani ambacho unataka.

Vilevile katika kuchagua vitu ambacho tunavyovitaka hatunabudi kuushirikisha ubongo katika kufanya tafakari makini juu ya kitu ambacho tunavyovitaka.
Hivyo katika kufanya uchaguzi wa mambo ambayo unayoyataka lazima ujiulize maswali yafuatayo :

Unataka nini au unataka kuwa nani ?
Je ni sifa zipi ambazo zinazohitajika ili kuwa hivyo ambavyo unataka?
Je fursa zipi zinapatikana katika jambo hilo?
Je changamoto gani ambazo zipo katika kukamilisha jambo hilo?
Je ni nani ambaye atakusaidia katika jambo hilo?
Hayo ni baadhi ya maswali msingi ya kujiuliza katika kufanya kufanya uchaguzi wa jambo ambalo unalitaka.
Mpaka kufikia hapo sina la ziada endelea kutembelea Muungwana blog kila wakati.

Na. Benson Chonya.
logoblog

Thanks for reading Mambo yatakayokusaidia kuwa Chanya katika maisha yako

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment