ADS

Nov 28, 2021

RC Telack awakumbusha na kuwahimiza jambo wazazi na walezi.

  Muungwana Blog       Nov 28, 2021

 


Na Ahmad Mmow, Lindi.

Wazazi na walezi mkoani Lindi wameaswa wajitahidi kuhakikisha watoto na vijana watambue uwepo wa Mungu.


Wito huo umetolewa leo mjini Lindi, na mkuu wa mkoa wa Lindi, Zainabu Telack alipozungumza na waumini wa madhebu mbalimbali ya dini waolikutana kwaajili ya kuliombea dua taifa na kushuru kwa Tanzania bara kufikisha miaka 60 ya Uhuru.


Telack alisema wazazi na walezi hawana budi kufanya kazi ya kuwafanya vijana na   watoto wamtambue Mungu, wajue uwepo na kazi zake.


Alibainisha kwamba kizazi cha sasa kinapita katika kipindi kigumu kutokanana kukua kwa teknolojia. Hali inayosababisha vijana na watoto wengi kupita kwenye njia zisizo mpendeza Mungu.


Telack ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kusanyiko hilo alisema njia wanazopitia vijana na watoto ndizo zinazosababisha vitendo visivyokubalika katika maadili na utu. Hasa matumizi mabaya ya mitandao.


Maandalizi ya dua, shukrani na maombi hayo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa mtakatifu Andrea Kagwa yamefanywa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Lindi kwa ajili ya wananchi wa wilaya ya Lindi.


logoblog

Thanks for reading RC Telack awakumbusha na kuwahimiza jambo wazazi na walezi.

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment