Ticker

6/recent/ticker-posts

Tetesi za soka Ulaya Jumamosi tarehe 20.11.2021

 


Manchester United inapanga kumuachilia kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba, 28, aondoke, huku akiwa na uwezekano mkubwa wa kwenda Real Madrid. (Marca via Sport Witness)


Kiungo wa kati wa Manchester United na England Jesse Lingard huenda akawa njiani kuelekea West Ham katika mwezi wa Januari mwakano kwa mkataba wa pauni milioni 10. Mazungumzo ya mkataba baina ya Manchester United na mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 28-yalivunjika hivi karibuni, huku David Moyes akiwa makini kusaini mkataba na Lingard wa kudumu. (Sun)Meneja wa Tottenham Antonio Conte pia anania ya kusaini mkataba na mchezaji huyo wa United kwa uhamisho wa bila malipo msimu ujao . (Express)


Manchester United wana nia ya kusaini mkataba na mchezaji wa klabu ya Atletico Madrid Kieran Trippier. United wanajiandaa mlinzi kumuuza Diogo Dalot, 22, kwa Roma iwapo beki huyo wa England mwenye umri wa miaka 31 atajiunga na kikosi hicho. (Manchester Evening News)


Walinzi wa Chelsea Cesar Azpilicueta na Andreas Christensen wanalengwa kuhamishwa na Xavi ambaye anataka kuwaleta wawili hao katika Barcelona kwa uhamisho huru. Mikataba ya Azpilicueta, na Christensen mweye umri wa miaka 32, na yote inamalizika msimu ujao. (Express)West Ham wana nia na kiungo wa safu ya kati-nyuma wa Ujerumani na Hertha Berlin Niklas Stark, mwenye umri wa miaka 26. (Sport1 via Team Talk)


Meneija wa Burnley Sean Dyche anasema kiungo wa safu ya Kati -nyuma Muingereza James Tarkowski, 28, ana "mawazo ya wazi " na "malengo" licha ya kwamba klabu za Newcastle, West Ham na Tottenham zinamtaka. (Burnley Express)Arsenal wameafiki mkataba wa kumruhusu kiungo wa kati Misri Mohamed Elneny, 29, kwenda Galatasaray. (Vatan via Express)Winga wa Chelsea Christian Pulisic huenda akaelekea Liverpool kwani muda wa mchezo anaopewa Mmarekani huyo katika timu hiyo unaendelea kuwa mfupi katika Stamford Bridge. (Star)


Spurs pia wameonyesha nia kwa kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ufaransa Corentin Tolisso lakini wanaweza kukabiliwana na ushindani kutoka kwa Internazionale ambao pia wanamvuizia mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 27. (Kicker - in German)Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amekanusha taarifa kuhusu kuihama timu hiyo kwa deni kwa mlinzi Mwales Neco Williams mwenye umri wa miaka 20. Licha ya tetesi kwamba hatakuwa katika Anfield siku zijazo, Klopp amedokeza kwamba huenda kukawa na nafasi yake katika kikosi hicho. (Mirror)


Chelsea wanajiandaa kumhamisha kiungo wa kati wa Barcelona mwenye umri wa miaka 17 Gavi. Mhispania huyo ambaye mkataba wake unaendelea hadi 2023, ameondoa kipengele cha kumuachilia cha paumi milioni 42 huku Chelsea wakiangalia jinsi ya kumhamisha. (Sun)Post a Comment

0 Comments