Nov 25, 2021

Wahamiaji 31 wafa maji baada ya boti yao kuzama Calais

  Muungwana Blog       Nov 25, 2021

 


Calais,Wahamiaji wapatao 31 waliokuwa njiani kuelekea Uingereza wamekufa baada ya boti yao kuzama katika mlango wa bahari wa kuingilia Uingereza. 


Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Gerald Darmanin amesema vifo hivyo ni janga kubwa zaidi la wahamiaji wanaofanya safari hatari za baharini kujaribu kuingia Ulaya. 


Darmanin amesema watu 34 wanaaminika kuwepo kwenye boti hiyo. Hata hivyo mamlaka imepata miili 31, ikiwemo wanawake watano na msichana mdogo pamoja na manusura wawili. 


Mtu mmoja hajulikani alipo. Uraia wa watu hao pia haukujulikana mara moja. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameapa kutoruhusu eneo hilo la mlango wa bahari kati ya Ufaransa na Uingereza kuwa makaburi. Macron ameitisha mkutano wa dharura na mawaziri wa Ulaya kujadili juu ya kadhia hiyo.


logoblog

Thanks for reading Wahamiaji 31 wafa maji baada ya boti yao kuzama Calais

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment