ADS

Nov 28, 2021

Waziri mkuu wa zamani wa Cambodia afariki dunia

  Muungwana Blog       Nov 28, 2021


Waziri Mkuu wa zamani wa Cambodia, Mwanamfalme Norodom Ranariddh, amefariki dunia nchini Ufaransa. 


Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa waziri wa habari wa Cambodia, ambaye ameisambaza kupitia ukurasa wa Facebook.Chama cha siasa cha Mwanamfalme Ranariddh aliyekuwa na umri wa miaka 77 kilishinda uchaguzi wa mwaka 1993, na aliondolewa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi ya 1997.


Mapinduzi hayo yalifanywa na mshirika wake wa muungano na hasimu wa kisiasa, Hun Sen, ambaye alisalia madarakani kama waziri mkuu wa Cambodia kwa zaidi ya miaka 20.

logoblog

Thanks for reading Waziri mkuu wa zamani wa Cambodia afariki dunia

Previous
« Prev Post

No comments:

Post a Comment