Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Yanga kuvunja benki kumsajili Clatous Chama

 


Vyanzo kutoka nchini Ghana vinaripoti kuwa, Klabu ya Yanga ipo tayari kutoa kiasi cha shilingi bilioni moja ili kumsajili kiungo wa zamani wa Simba SC, Clatous Chama anayekipiga kwenye klabu ya RS Berkaine ya Morocco.


Taarifa hizo zimeripotiwa kutoka kwa Mwanahabari wa michezo nchini Ghana, Micky Jr ambaye ameandika kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii kuwa, pamoja na dau hilo lakini Chama yupo tayari kijiunga na Simba na sio Yanga.


Micky Jr ameandika kuwa; “Naelewa YangaSCwapo tayari kulipa kiasi kinacho karibia shilingi bilioni moja kwa Clatous Chama na wakala wake ili achague kujiunga nao na sio Simba SC”.


“Chama anataka kurejea Simba ambapo alichukuliwa kama mfalme. Mwenyekiti wa Simba alipokea simu kuyoka kwa Chama wiki mbili zilizopita” ameandika Micky Jr.


Taarifa hizo zimeshika kiasi kutokana na Chama kupata wakati mgumu wa kuzoea mazingira ya nchini Morocco jambo linalomfanya akose nafasi ya uhakika kwenye kikosi cha kwanza chini ya Kocha Florent Ibenge.


Chama amekosa michezo michezo mitatu mfululizo ya RS Berkaine huku miwili ya iliyopita alikuwa anatokea benchi ilhali Tuisila kisinda winga aliyetokea Yanga amekuwa akipata nafasi mara nyingi kucheza

Post a Comment

0 Comments