Ticker

6/recent/ticker-posts

Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza (MPC) wametoa shukrani kwa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania

 


Na Maridhia Ngemela, Mwanza

Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Mwanza(MPC) kimetoa taarifa ya waandishi wa habari waliopata majeruhi katika ajari iliyotokea  tarehe 11 mwezi Januari mwaka huu waliokuwa katika msafara wa Mkuu wa mkoa wa Mwanza Muhandisi Robert Gabriel.


Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari Edwin Soko amesema kuwa madaktari wa hospital ya Kanda ya Bugando wamethibisha kuwa majeruhi hao ambao ni Tunu Hermani na Vanni Charles wanaendelea vizuri na matibabu yote watayapatia hospitali hapo kutokana na kuwa na vifaa vya matibabu vyenye ubora na uhakika.


Amesema kuwa majeruhi hao wanaendelea vizuri wako mikono salama ya uangalizi hivyo wananchi waamini vyanzo vya habari na waachane na maneno ya mitaani.


Hata hivyo amemshukru Rais  wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Waziri  wa Habari na viongozi wa mkoa wa Mwanza kwa kutoa  ushirikiano kwenye tatizo hilo.

Post a Comment

0 Comments