Ticker

6/recent/ticker-posts

Duwasa Yatangaza Donge Nono Atakayefichua Wezi Wa Mita


MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), imetangaza donge nono la Sh 500,000 kwa atakayefi - chua wezi na waharibifu wa mita za maji.


Taarifa iliyotolewa jana jijini hapa na Mkuu wa Kitendo cha Mawasiliano cha Duwasa, Sebastian Warioba ilibainisha kuwa hatua hiyo imetokana na kukithiri wizi na uharibifu wa mita za maji. Alisema vitendo hivyo vimekuwa vikisababisha hasara na usumbufu kwa mamlaka na wateja.


“Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma inatangaza donge nono la shilingi 500,000 kwa yeyote atakayetoa taarifa sahihi itakayowezesha kukamatwa kwa wezi na waharibifu wa mita za maji…Taarifa hiyo itolewe kwa kuwasiliana na Mkurugenzi Mtendaji au kwa simu namba 0756162432,” alisema.


Warioba alisema katika kutoa taarifa hizo, ni lazima zibainishe mtu au watu wanaoharibu au kuhusika na wizi huo.


Aliongeza: “Pia taarifa ibainishe mita zinazoibiwa zinapelekwa wapi na kwa malengo gani na zile mita zinazoharibiwa zinaharibiwa kwa malengo gani.” Alihadharisha wananchi kutokubali kufungiwa mita zisizotambulika Duwasa. 

Post a Comment

0 Comments