Ticker

6/recent/ticker-posts

Faida 11 za Push Up kiafya unazotakiwa kuzijua

  


Mazoezi ni njia moja wapo ya kutufanya tuwe vizuri na wenye afya njema. Kama unahitaji zoezi ambalo litanufaisha sehemu mbalimbali za mwili wako, push ups ni zoezi moja wapo. Push up ni zoezi ambalo linaweza kufanywa na wanaume na wanawake bila gharama yoyote; na faida zake ni zaidi ya kunyoosha tu misuli.

Naamini unapenda afya njema pamoja na maarifa; fuatilia makala hii nikufahamishe faida 11 za zoezi la push up kiafya ikiwa utalifanya mara kwa mara.

1. Huboresha mkao na mwonekano wako

Push up ni njia bora ya kuufanya mgongo wako unyooke. Push up huimarisha na kuweka sehemu mbalimbali za mwili wako kukaa jinsi ipasavyo; kwa njiaa hii huufanya mwili wako uwe na mwonekano mzuri.

2. Huimarisha misuli

Unapopiga push up unahusisha misuli mbalimbali kwenye mwili wako; misuli hii ni kama ile ya mikono, kifua na miguu. Kwa njia ya mazoezi ya push up utaweza kuimarisha misuli hii vyema.

3. Huimarisha mifupa

Mifupa nayo hutumika katika mchakato wa zoezi zima la push up. Kupiga push up kutaifanya mifupa yako kuimarika na kuwa yenye afya zaidi; uzito na uimara wa mifupa unaweza kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na zoezi la push up ikiwa utafanya mara kwa mara.

4. Huboresha metaboli

Metaboli ni mchakato ambao mwili hutumia virutubisho vinavyopatikana kwenye chakula ili kuupa mwili nguvu. Kwa njia ya kufanya mazoezi ya push up utawezesha mchakato huu kwenda vyema.

5. Huongeza kifua

Kama nilivyoeleza hapo awali kuwa push up huimarisha misuli mbalimbali ikiwemo ya kifua, ni wazi kuwa misuli hii ikijengeka vizuri hata umbo la kifua chako litakuwa kubwa na zuri.

6. Huunda tumbo vizuri

Je unafahamu juu ya six-parks? Ikiwa unatamani kuwa na kifua na tumbo lenye mwonekano wa six-parks basi push up ni moja kati ya zoezi litakalokuwezesha kufikia lengo lako.

7. Hukusaidia kupunguza uzito

Mazoezi ni njia moja wapo ya kupunguza uzito kwani huunguza kalori na mafuta mengi mwilini. Push up ni zoezi ambalo likifanywa kwa usahihi linaweza kupunguza kiasi kikubwa cha uzito mwilini mwako.

8. Huondoa maumivu ya mgongo

Push up huimarisha misuli ya maeneo ya tumbo, mgongo na hata eneo la uti wa mgongo na kukufanya kuwa na misuli yenye afya zaidi. Ikiwa unafanya kazi nyingi zinazohitaji kubeba vitu, basi push up zitakuwezesha kujikinga na maumivu ya mgongo.

9. Huzuia maumivu ya shingo na mabega

Misuli ya shingo na mabega huhusishwa kwa kiasi fulani katika zoezi la push up. Hivyo zoezi hili huongeza mjongeo mzuri zaidi kwenye viungio vya mabega na shingo, hivyo kuzuia maumizu ya shingo na mabega.

10. Hukuongezea usawa wa mwili (balance)

Zoezi la push up hukuwezesha uweze kuwa na usawa zaidi kwenye mwili wako wakati wa mijongeo. Hii ni kutokana na misuli mbalimbali kuimarishwa na kuhusika wakati wa zoezi hili.

11. Hunufaisha mwili mzima

Push up ni zoezi linalonufaisha mwili mzina na wala si misuli ya mikono, kifua na tumbo pekee. Zoezi hili huhamasisha mzunguko mzuri wa damu pamoja na uzalishaji wa homoni mbalimbali ambazo hulidha afya ya miili yetu.

Neno la Mwisho

Ni wazi kuwa push up ni zoezi zuri sana ambalo unaweza kulifanya bila gharama au kifaa cha ziada. Jambo la kuzingatia ni kuhakikisha unafanya zoezi hili katika mazingira salama na kwa kiasi kinachotakiwa.

Post a Comment

0 Comments