Ticker

6/recent/ticker-posts

Guterres aitaka Mali kutangaza tarehe ya uchaguzi


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameutaka utawala wa kijeshi nchini Mali kutangaza tarehe ya uchaguzi. Guterres ameelezea wasiwasi wake mkubwa kutokana na serikali hiyo kutangaza kuwa uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi ujao utaahirishwa hadi mwaka 2026.


 Amewaambia waandishi habari ana matumaini kwamba atafanikiwa kuwasiliana hivi karibuni na serikali ya kijeshi ya Mali na anaamini ni muhimu kabisa kwa serikali ya Mali kuwasilisha ratiba ya uchaguzi.


 Amesema anashirikiana na Jumuiya ya Uchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS na Umoja wa Afrika kuandaa mazingira ambayo yataiwezesha serikali ya Mali kuchukua msimamo unaofaa na unaokubalika ili kuharakisha kipindi cha mpito ambacho tayari kimeanza muda mrefu. 


Baada ya miezi kadhaa ya mvutano wa kidiplomasia, wiki iliyopita ECOWAS ilikubaliana kufunga mipaka yake na taifa hilo la Ukanda wa Sahel na kuliwekea vikwazo vya kibiashara.

Post a Comment

0 Comments