Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Mali: Jeshi latuhumiwa kwa mauaji mapya dhidi ya raia


Wakati ushahidi wa kupelekwa kwa wapiganaji wa Urusi nchini Mali ukiongezeka, jeshi la taifa linashutumiwa kwa mauaji mapya. Kwa mujibu wa duru kutoka nchini Mlai na kimataifa, wanajeshi wa Mali wamehusika na vifo vya zaidi ya raia 15 katika maeneo kadhaa katikati mwa nchi katika muda wa wiki moja iliyopita.


Jeshi la Mali linakanusha shutuma hizi na limebaini kwamba lilifanya operesheni za kukabiliana na ugaidi.


Tukio la kwanza lilianza Desemba 31, wiki moja iliyopita, wakati operesheni ya jeshi la Mali katika wilaya za Nara na Banamba, mkoa wa Koulikouro, karibu na mpaka wa Mauritania, ilisababisha raia kati ya 18 na 23 kuuawa kikatili, kulingana na vyanzo kadhaa. Shirika la Haki za Binadamu kwa Jumuiya za Kichungaji za Kisal, na wanaharakati wa haki za binadamu kutoka Mali na kimataifa, wanataja ugunduzi wa makaburi ya halaiki.


Tukio la pili: Jumatatu iliyopita, Januari 3, huko Guiré, katika eneo hilohilo. Vyanzo vingi vya kutoka Mali na kimataifa vinaripoti kukamatwa kiholela na angalau raia wawili waliuawa. Katika taarifa ya Jumatano tarehe 5 na ambayo ilitolewa Alhamisi, jeshi la Mali linadai kuwa lilifanya mashambulizi ya anga katika eneo hilo asubuhi kabla ya kuwakamata, baadaye siku hiyo hiyo, "washukiwa wanne walijeruhiwa katika mapigano".


Kufungwa na kupigwa

Tukio la tatu: Jumanne Januari 4, siku tatu zilizopita, huko Nia Wouro, karibu na Bandiagara, katika eneo la Dogon. Hapa tena, hizi ni shuhuda za ndani zilizokaguliwa na watafiti, kitaifa na kimataifa, wakichunguza hali ya usalama katika maeneo haya, ambapo wanashtumu kitendo cha jeshi la Mali, Fama, ambapo washambuliaji walifungwa na kupigwa. Baadhi ya vyanzo vinasema watu wanne waliuawa.


Katika taarifa hiyo hiyo, jeshi la Mali linajibu shutuma hizo na kusisitiza kwamba operesheni mbili katika sekta hii ya Sofara-Bandiagara zimewezesha kuzima mashambulizi ya kigaidi.


Hatimaye, makao makuu ya jeshi wanashutumu "habari zisizo na msingi" ambazo zinahusisha "baadhi ya wahusika" "wepesi wa kukashifu Fama".

Post a Comment

0 Comments