Ticker

6/recent/ticker-posts

RUNALI kutatua changamoto ya vifungashio.


Na Ahmad Mmow, Nachingwea. 

Chama kikuu cha ushirika cha RUNALI ambacho kinaundwa na vyama vya msingi vya ushirika (AMCO) vilivyopo katika wilaya za Ruangwa, Liwale na Nachingwea kipo kwenye mpango wa kununua vifungashio badala ya kutumia wazabuni. 


Hayo yalielezwa jana na meneja mkuu wa RUNALI, Jahida Hassan baada ya kukamilika mnada wa 11  wa korosho kwa msimu wa 2021/2022 ambao ni wa mwisho.


Jahida alisema kwa misimu mingi kumekuwa na changamoto ya vifungashio kutokanana kuwatumia wazabuni. 


Kwahiyo ili kuondokana na changamoto hiyo kimejipanga kuanza kununua vifungashio. " Matarajio yetu nikwamba msimu wa ufuta tutatumia vifungashio ambavyo vitanunuliwa na RUNALI yenyewe. Tutaanza mchakato wa kupata kibali cha kununua wenyewe.


Kwahiyo matarajio yetu msimu wa ufuta tutumia vifungashio tutakavyo nunua wenyewe. Tupo kwenye mchakato wakuomba kibali kitakacho tuwezesha kununua,"alisema Jahida.


Aidha alisema ununuzi wa zao hilo haukuwa na changamoto nyingi ikilinganishwa na misimu iliyopita. Huku akiweka wazi kwamba lengo la ukasanyaji kwa msimu huu limefikia asilimia tisini na saba. Kwani lengo lilikuwa ni kukusanya tani 48,000, hata hivyo zimek usanywa tani 46,000. 


Mbali na hayo, meneja mkuu  huyo  aliitaja changamoto kubwa iliyojitokeza katika msimu huu ni baadhi ya wakulima akaunti zao kulala kutokanana wakulima kutoa fedha zote kila msimu. Alisema hali hiyo inasababisha wafanye mchakato wa kuzindua akaunti hizo. 


" Kwahiyo wanapoingiziwa fedha zao wanashindwa kutoa na kuanza kulalamika. Wito wangu kwa wakulima wasitoe fedha zote," Jahida alisisitiza. 


Msimu wa 2021/2022 ulifungwa jana kukiwa kumefanyika minada 18 kwa vyama vikuu viwili vyote vilivyopo katika mkoa wa Lindi ambavyo ni RUNALI na Lindi Mwambao.

Post a Comment

0 Comments