Ticker

6/recent/ticker-posts

WHO yaongeza dawa nyingine kutibu virusi vya Corona


Shirika la afya duniani, WHO, kwa mara nyingine limeidhinisha dawa nyingine 2 zaidi zinazoweza kutumiwa kutibu virusi vya Corona.


Tangazo la WHO limekuja wakati huu hospital nyingi duniani zikianza kupokea idade kubwa ya wagonjwa, huku likitabiri kuwa huenda katika kipindi cha miezi 6 ijayo, karibu nusu ya raia wa bara Ulaya watakuwa wameambukizwa virusi vya Omicron;


Miongoni mwa dawa zilizokuwa zimependekezwa na jarida la kitabibu la Uingereza ni pamoja na dawa aina ya baricitinib kwa kuchangaya na corticosteroids zinazotumika kutibu magonjwa ya mfumo wa upumuaji unaosababisha athari za viungo, ambapo inaweza kutumika kwa wagonjwa wa Covid 19 walio katika hali mahututi.


Dawa nyingine ni Sotrovimab, ambayo inapendekezwa kutumiwa kwa wagonjwa ambao hawahitaji hewa ya Oxygen wala kulazwa hospitalini, na zaidi inapendekezwa kutumika kwa wazee na watu wenye ugonjwa wa Kisukari.


Mpaka sasa WHO imesharuhusu kutumika kwa dawa aina 3 ikiwemo nyingine inayofahamika kama Tocilizumab na Sarilumab zilizoidhinishwa mwezi Julai mwaka jana.


Dawa za matibabu zinazothibitishwa na shirika la afya duniani WHO, taarifa zake huwa zinaboreshwa mara kwa mara baada ya kupokea takwimu kuhusu majaribio yaliyofanyika kuthibitisha ufanisi wake.

Post a Comment

0 Comments