Ticker

6/recent/ticker-posts

 


Rais Samia atoa maagizo kupanda kwa bei ya mafuta

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameitisha Kikao cha dharura usiku wa jana tarehe 08 Mei Ikulu ya Dar es Salaam kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta nchini.


Miongoni mwa waliohudhuria kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata na makatibu wakuu wao.


Katika kikao hicho, Rais Samia amewaagiza viongozi hao kutafuta suluhisho la haraka  katika kukabiliana na tatizo hilo la Upandaji wa bei ya Mafuta nchini.

Post a Comment

0 Comments