Trump achunguzwa kwa kuvunja Sheria ya Ujasusi


Shirika la Ujasusi wa ndani la Marekani, FBI, limegunduwa nyaraka zenye siri nzito za serikali ndani ya kasri la rais wa zamani, Donald Trump, kwa mujibu wa hati mpya za mahakama zilizochapishwa jana.


 Maafisa wa FBI walivamia kasri la Mar-a-Lago ambalo ni makaazi binafsi ya Trump siku ya Jumatatu, lakini hawajasema hadi sasa kile walichokigunduwa. 


Maafisa hao walichukuwa zaidi ya masanduku 20, pamoja na vitabu vya picha, taarifa kumuhusu rais wa Ufaransa, na karatasi iliyoandikwa kwa mkono. Kwa mujibu ya hati za mahakama, kulikuwa na seti 11 za nyaraka za siri za serikali, nne kati yao zikiwa na alama ya "siri nzito". 


Moja kati ya nne hizo ilipewa kiwango cha juu kabisa cha siri za masuala ya usalama. Kwa mujibu wa hati hizo za mahakama, Trump sasa anachunguzwa chini ya Sheria ya Ujasusi, sheria ambayo alipokuwa rais aliiongezea adhabu zaidi kwa wanaoivunja.

Post a Comment

0 Comments