F Jinsi Zelensky anavyopambana na changamoto ya vita vya Magharibi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Jinsi Zelensky anavyopambana na changamoto ya vita vya Magharibi


Mahusiano yao yanaweza kuwa karibu, kupeana mikono kunaweza kuwa thabiti, lakini Rais Volodymyr Zelensky alilazimika kukunja mikono yake juu wakati wa safari yake ya Marekani na Canada.


Mwisho ulikuwa rahisi zaidi.


Waziri Mkuu Justin Trudeau aliahidi kuunga mkono Ukraine "haijalishi ni muda mrefu kiasi gani itachukua" dhidi ya uvamizi wa Urusi, na ana uungwaji mkono wa pande zote katika juhudi hiyo.


Msaada wa Marekani ni mkubwa zaidi, lakini siasa zake ni ngumu zaidi.


Rais Zelensky alipata kifurushi kingine cha kijeshi cha $325m (£265m) kutoka Ikulu ya Marekani, lakini haikuwa $24bn ambazo alitarajia.


Pendekezo hilo halikupita katika Congress kwasababu ya kutokubaliana juu ya bajeti.


Ugumu hauishii hapo pia.


Kando na mwenzake Joe Biden, kiongozi wa Ukraine pia alikuwa na mikutano na wanasiasa wa chama cha Republican ambao wanajitahidi kuzuia mashaka yanayoongezeka katika chama chao.


"Tunalinda ulimwengu wa kiliberali, ambao unapaswa kuwa kwendana na Republican," mshauri wa serikali huko Kyiv anasema.


"Ilikuwa ngumu zaidi wakati vita vilipoanza, kwa sababu ilikuwa ni machafuko," anasema.


"Sasa tunaweza kuwa mahususi zaidi na maswali yetu, kwani tunajua washirika wetu wana nini na wanaihifadhi wapi. Rais wetu anaweza kuwa waziri wa ulinzi katika nchi kadhaa!"


Ala! Kumbe sio hivyo kwa Kyiv na changamoto za kisiasa zinaongezeka.


"Kwa nini Ukraine iendelee kuwa na uhuru wa kifedha? Muonekano wa ushindi ukoje?"


Haya yote ni maswali ambayo kiongozi wa Ukraine amekuwa akijaribu kujibu kwenye jukwaa la dunia.


Na hii ndiyo sababu sasa anaonekana kufanya mazungumzo zaidi kuliko kufanya kampeni - ili tu usaidizi wa Magharibi uendelee kuingia.


Yote katika wiki moja ambapo Kyiv ilikosana na mmoja wa washirika wake waaminifu zaidi Poland, katika mzozo juu ya nafaka ya Ukraine.


Marufuku ya Poland ya uagizaji wa bidhaa kutoka Ukraine ilipelekea Rais Zelensky kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuishutumu Warsaw kwa "kuisaidia Urusi".


Wacha tuseme kwamba hili lilichukua mkondo mbaya sana huko Poland, huku Rais Andrzej Duda akielezea Ukraine kama "mtu anayezama ambaye anaweza kukuvuta na wewe pia".


Hali kwa sasa imeendelea kutulia.


"Ukraine inapaswa kuangalia kuendeleza maslahi yake, kwa kila namna, huku ikizingatia hali katika nchi washirika na EU. Ni changamoto."


Hizi ni aina za mizunguko ya kidemokrasia ambayo kiongozi wa Urusi Vladimir Putin hahitaji kuwa na wasiwasi nayo.


Ndio maana Kyiv inajaribu kuonyesha vita hivi kama vita sio tu kwa uhuru wake, lakini kwa demokrasia yenyewe.

Post a Comment

0 Comments