F Kosovo na Serbia zazozana juu ya makabiliano ya bunduki katika nyumba ya watawa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Kosovo na Serbia zazozana juu ya makabiliano ya bunduki katika nyumba ya watawa

 


Kosovo na Serbia zinazozana katika mzozo mbaya kati ya washambuliaji wa kabila la Waserb na polisi kaskazini mwa Kosovo.


Polisi mmoja na watu watatu wenye silaha waliuawa wakati shambulio dhidi ya nyumba ya watawa wa dini ya Orthodox ya Serbia katika kijiji cha Banjska siku ya Jumapili.


Waziri Mkuu wa Kosovo Albin Kurti aliishutumu Serbia kwa kuunga mkono kundi hilo lenye silaha.


Rais wa Serbia Aleksandar Vucic alisema maafisa wa Kosovo waliwajibika kwa vifo hivyo.


Alisema washambuliaji watatu waliouawa walikuwa Waserbia wa Kosovo.


Mapigano ya Jumapili yanaashiria moja ya hali mbaya zaidi nchini Kosovo kwa miaka, na yanafuatia miezi kadhaa ya mvutano unaoendelea kuongezeka kati ya pande hizo mbili.


Kosovo ilijitangazia uhuru wake mwaka 2008 lakini Serbia - pamoja na washirika wakuu wa Belgrade -China na Urusi - hawaitambui.


Waserbia wengi wanaiona Kosovo kama mahali pa kuzaliwa kwa taifa lao. Lakini kati ya watu milioni 1.8 wanaoishi Kosovo, 92% ni wa jamii ya kikabila ya Waalbania na 6% tu ni wa kabila la Waserbia.

Post a Comment

0 Comments