F Mwili wa mwanamke uliopatikana mdomoni mwa mamba mwenye urefu wa futi 13 umetambuliwa | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mwili wa mwanamke uliopatikana mdomoni mwa mamba mwenye urefu wa futi 13 umetambuliwa

 


Mamba mwenye urefu wa futi 13 (m 4) ameuawa, polisi wanasema, baada ya kuonekana huko Florida na mabaki ya mwanamke kwenye taya zake.


Mu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo aliviambia vyombo vya habari kuwa alimuona mamba kwenye mfereji wa Largo akiwa ameshikilia kiwiliwili cha chini mdomoni mwake.


Ofisi ya Sherifu wa Kaunti ya Pinellas ilisema mnyama huyo aliuawa na kuthibitisha kuwa mabaki ya Sabrina Peckham mwenye umri wa miaka 41 yalipatikana kwenye njia ya maji.


Uchunguzi utabainisha mazingira yaliyosababisha kifo cha mwanamke huyo.


Polisi walisema maafisa wao waliitwa sab ana dakika hamisini mchana kwa saa za eneo siku ya Ijumaa baada ya ripoti ya mwili kuonekana kwenye njia ya maji.


Jamarcus Bullard alisema alikuwa akienda kwenye mahojiano ya kazi alipomwona mamba huyo akiwa na kiwiliwili mdomoni mwake.


"Niligundua kuwa alikuwa na mwili mdomoni - kama kiwiliwili cha chini - kwa hivyo nilipoona kwamba nilikimbia moja kwa moja hadi kwa idara ya zima moto," aliamwambia mtangazaji wa Fox 13.

Post a Comment

0 Comments