Sheria mpya za biashara baada ya kuondoka kwa Uingereza katika Muungano wa Ulaya au Brexit, zinazohusu magari ya umeme zinaweza kuwagharimu watengenezaji wa Ulaya pauni bilioni 3.75 katika miaka mitatu ijayo, shirika la tasnia limesema.
Sheria hizo zinakusudiwa kuhakikisha kuwa magari ya umeme yanayozalishwa na Umoja wa Ulaya yanatengenezwa kwa kutumia vipuli vingi vinavyotoka ndani.
Lakini watengenezaji wa pande zote wanasema hawako tayari.
Jumuiya ya Watengenezaji Magari ya Ulaya (ACEA) pia ilionya kua hatua hizo zinaweza kupunguza mapato kutoka kwenye viwanda vya EU kwa magari 480,000.Na walisema wateja watalipia gharama.
Tatizo kuu liko katika kile kinachoitwa "sheria za asili" ambazo zinaanza kutumika Januari. Zinatumika kwa usafirishaji wa magari kote chini ya masharti ya mkataba wa Brexit, Mkataba wa Biashara na Ushirikiano wa Uingereza na EU.
Watahakikisha kwamba magari ya umeme yatahitaji kuwa na betri zinazozalishwa nchini Uingereza au EU.
Magari ambayo hayatimizi vigezo yatatozwa ushuru wa 10% yanaposafirishwa kupitia vituo vya safari za magari katika pande zote mbili.
0 Comments